TAREHE YA
KUANZISHWA KWA SHIRIKA:
Shirika la
BUFADESO lilianzishwa Tarehe 27/02/2012
USAJILI:
Shirika limesajiliwa mnamo tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696 chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya kiserikali.

DIRA
YA SHIRIKA:
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda
DHAMIRA YA SHIRIKA:
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu
LENGO KUU:
Kuwa na wakulima wanaotumia na kunufaika na mbinu bora za kilimo ifikapo 2025
Kuwa na wakulima wanaotumia na kunufaika na mbinu bora za kilimo ifikapo 2025
MALENGO MADOGO MADOGO:
1) Kuwa na wakulima wanaotumia mbinu bora za kilimo ifikapo 2018
2) Ongezeko la kaya za wakulima na wafugaji wanaotumia mbinu za kilimo bora ifikapo 2017
3) Uwepo wa wakulima na wafugaji wanaojishughulisha na kunufaika na kilimo biashara ifikapo 2018.
4) Kuwa na wakulima wanaohifadhi mazingira na wanaoweza kukabiliana na athari za mabadiriko ya hali ya hewa ifikapo 2019
5) Kuwa na vikundi vyenye shughuli na miradi endelevu ifikapo 2017.
SHUGHULI ZA SHIRIKA:
i. Kutoa Elimu na mafunzo kwa wanachama
ii. Kuratibu shughuli za wanachama wa shirika.
iii. Ushawishi na utetezi katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kimazingira ili kuleta maendeleo endelevu kwa jamii na wanachama
iv. Kuwakilisha wanachama kwenye ngazi za juu.
v. Kuhamasisha masuala mtambuka hasa UKIMWI/VVU na usawa wa kijinsia.
MAADILI YA SHIRIKA:
Utendaji kazi utajikita katika viwango
vifuatavyo:-
i.
Uaminifu.
ii.
Heshima na
kuthaminiana.
iii.
Ushirikiano.
iv.
Kuzingatia na
kujali muda.
v.
Kutozingatia
ubaguzi wa aina yoyote
vi.
Kudhibiti
rushwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni