Jumanne, 30 Agosti 2016

MFUMO WA KUWEKA NA KUKOPA HISA

HISA
Maana ya HISA
Ni mpango wa mtu, kikundi au kampuni kuuza au kununua kitu chenye thamani fulani kwa lengo la kujipatia faida


FAIDA YA NJIA HII
  • Hakuna haja ya kukopa fedha kutoka nje wakati jamii ina uwezo wa kupata fedha yenyewe
  • Njia ya kuweka fedha na kukopeshana ni ya uwazi
  • Riba inayopatikana inakuwa ni ya wanakikundi na siyo shirika fulani
  • Nguvu ya kikundi inahamasisha mwachama kurudisha fedha kwa muda uliokubalika kikatiba
  • Utafanya mwanakikundi kufanya kazi kwa bidii
  • Kujiunga kwenye vikundi vya HISA haizuii kujiunga ktk vikundi vingine
  • Utaratibu wa kugawana unaruhusu mwanakikundi kutumia kiasi alichojiwekea kwa kufanya mipango yake ya baadae.


HASARA AU VIPINGAMIZI VYA MFUMO
  • Mwanzoni hela ya kukopa huwa haitoshi
  • Muda mfupi wa kukaa na mkopo
  • Mikopo inakuwa haipo kila wakati
  • Baada ya kugawana inalazimu kuanza upya


JINSI UTARATIBU HUU UNAVYOFANYA KAZI 
  • Utaratibu wa mfumo katika muundo huu (HISA) kuna awamu nne (4)


AWAMU YA KWANZA (I)
  • Ni awamu ya kuanzisha mfumo
  • Lengo ni kuchagua kikundi na kuingiza ktk tabia za mfumo huu. Awamu hii ni haraka kama kikundi kipo na na kinafanya kazi.


AWAMU YA PILI (II)
  • Ni awamu ya kukazia maarifa
  • Lengo ni kutoa mafunzo yatakayo kiimarisha kikundi


AWAMU YA TATU (III)
  • Ni awamu ya kuendeleza kikundi
  • Lengo ni kusaidia kikundi kiweza kuwa ktk hali ya kujitegemea na kujiendesha chenyewe

AWAMU YA NNE IV
  • Ni awamu ya mwisho kabisa
  • Lengo ni kukisaidia kikundi kiweze kujitegemea na kuachana na Mradi

JINSI MFUMO UNAVYOFANYA KAZI
  • Wanachama ndani ya kikundi wanatakiwa kuwa kati ya 15 – 30
  • Kikundi kinaweza kuwepo au kuundwa kikundi kipya wanakikundi wawe wamechagua wenyewe wanaweza kuwa wanawake au wanaume
  • Kamati iwe na mchanganyiko wa jinsia kama kikundi ni cha mchanganyiko wa wanaume na wanawake
  • Kiongozi wa kijiji, kitongoji au kata hawaruhusiwi kuingia kwenye kamati ila ushauri wao unakaribishwa

Kikundi cha HISA kina uongozi yaani kamati ya watu watano (5)
  • Mwenyekiti 1
  • Katibu 1
  • Mtunza fedha 1
  • Wahesabu fedha 2
Pia watakuwepo/watachaguliwa watunza funguo wawili ambao hawatakuwa kwenye kamati ya kikundi
  • Viongozi hawa watachaguliwa kwa mwaka na wanaweza kuondolewa tena kwa kikao cha 2/3 ya wajumbe
  • Kikundi cha HISA kitakuwa na sheria zake yaani katiba
  • Sheria hizi zitatungwa na kamati ya kikundi na kufadhiliwa na wanachama wote
  • Sheria zitaurahisishia uongozi kufanya kazi
  • Kila mwanachama atakabidhiwa sheria moja ya kukumbuka
  • Kila mkutano wajumbe wataambiwa kutaja sheria kwa wenzao kulingana na walivyopeana majukumu
  • Atakaye shindwa kutaja sheria yake atalipa faini
  • Hii ni kwa ajiri ya kukariri sheria ili baada ya miezi kila mshiriki azijue zote
Muda wa kukutana
  • Kikundi cha HISA kitakuwa kinakutana kila baada ya muda fulani
  • Wanakikundi wataamua wenyewe muda na siku ya kukutana
  • Wanashauriwa kukutana 2 au 4 kwa mwezi
  • Kikundi kipange tarehe au  siku za kukutana kwa mwezi
  • Kikundi kipange kitakuwa kinakutania wapi? na muda gani?
  • Muda wa kukutana unashauriwa kuwa saa 1.na dakika 30 isizidi saa 2.
  • Vikundi vya hisa  vinatakiwa kukubaliana juu ya mzunguko wa kufanya kazi.
  • Wanakikundi wanatakiwa kukubaliana juu ya mzunguko kabla ya kuanza kazi.
  • Makubaliano ya mzunguko yanategemea ni lini wanachama  walio wengi wanahitaji kiasi kikubwa cha fedha
  • Siku ya mwisho ya mzunguko wanachama wanatakiwa kujitoa au kuingia katika kikundi.



Thamani ya HISA .
  • Hupangwa na wanachama wenyewe.
  • Kiwango cha chini cha hisa ni shilingi 500/= na cha juu ni kutokana na maamuzi.
  • Unaruhusiwa hununua hisa 1-5.

VIFAA VYA HISA.
Boksi la Hisa.
Kufuri 3
Daftali kubwa (ledger book)
Bakuli au mifuko 4( hisa, faini, jamii)
Daftali za kawaida 3
Vitabu vya ununuzi na ukopaji.
Muhuri
Calculator 
Kalamu.
Rula, penseli na kidau.


MIKOPO
  • Mwanachama anatakiwa kukopa mara1-3   ya hisa zake.
  • Kikundi kinatakiwa kujigawa katika vikundi vidogo vidogo vya watu wa 5 waliochaguana wenyewe.
  • Kikundi hiki cha watu 5 kitamjadili mwanachama anayetaka kukopa mkopo na kumpitisha wakizingatia wingi wa mkopo na biashara/ mradi anaotaka kufanya.
  • Katibu atagawa kiasi cha pesa inayotakiwa  kukopwa na kugawa katika vikundi vidogo vidogo.
  • Maombi ya mkopo yatawakilishwa kwa katibu.
  • Vigezo vya mkopo huwekwa kutegemea watu watakaotakiwa kukopa.
  • Wanachama wajadili muda wa kukaa na mkopo.


JINSI YA KUREKODI WAKOPAJI .
  • Mkopo unapotolewa kiasi kinaingizwa katika leja (ledger book) ya mkopo ikionyesha.
  • Namba ya mkopo
  • Jina la mkopaji na sahihi yake .
  • Kiasi gani anakopa



.
  • Kipindi cha marejesho.
  • Sahihi ya katibu na mkopaji
  • Riba
  • Dhamana.
  • Tarehe ya kuchukua mkopo.
  • Sahihi ya katibu na mkopaji.
  • Baki.
  • Katibu akumbuke kurekodi katika kitabu cha mwanachama.


RIBA.
  • Riba ni makubaliano ya wanachama.
  • Riba ni vizuri iwe ndogo ili wengi wakope.
  • Katika utaratibu huu inashauriwa 5%-50% ila vikundi vilivyo vingi vina asilimia 5.
  • Wanakikundi wajadili jinsi ya kurudisha mkopo.
  • Kikundi kinaweza kujadili kuwa riba ilipwe kila mwezi na mkopo wenyewe utalipa mwisho wa mkopo
  • Kukaa na mkopo inashauriwa isizidi miezi 3.
  • Mfano wa riba inavyopatikana.(Riba = mkopo x asilimia iliyopangwa)
  • Riba itaanza kulipwa baada ya wiki 4 baada ya kukopa (mwezi)


MWISHO WA MZUNGUKO.
  • Hakikisha mikopo yote, riba, faini na hisa zinatakiwa ziwe zimelipwa.
  • Katibu atahesabu jumla ya pesa zote.
  • Pia atahesau idadi ya hisa zote.
  • Katibu atachukua idadi ya fedha zote na  atagawa kwa idadi ya hisa zote.
  • Katibu atajua thamani ya hisa mpya (kizidishio)
  • Kila mwanachama ataambiwa kuhakikisha idadi ya HISA zake zote kama ni sawa na zile zililzomo kwe ledger ya kikundi.
  • Idadi ya hisa za mwanachama zitazidishwa na idadi ya hisa mpya.
  • Mwanachama atakabidhiwa fedha zote  mihuri ndani ya kitabu cha mwanachama zitaonyeshwa  zimebaki 0 kama Hisa anzia.
  • Katika ledger ya kikundi itaonyeshwa 0 na mwanachama ataweka sahihi.
  • Wanakikundi watakubaliana kiasi cha kubakia kwenye mfuko.

 Kwa maelekezo zaidi usisite kutuuliza kupitia bofya hapa

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO