Jumamosi, 14 Mei 2016

MKUTANO MKUU WA MWAKA ULIOFANYIKA TAREHE 14/05/2016

Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Mwaka katika eneo la Mkutano Shule ya Sekondari Sazira

Viongozi wa Shirika la BUFADESO

                       Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la                                         BUFADESO


                              Wasimamizi wa Uchaguzi wakihesabu kura za                                wagombea nafasi za uongozi wa Shirika.

                        Msimamizi wa Uchaguzi akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa
                                                    Wajumbe wa katika Kikao

                                  Mratibu wa Shirika Ndg. Baraka Kamese akitoa maelezo ya mikakati ya shirika 

Mkutano mkuu wa shirika la BUFADESO kwa mwaka huu umefanyika leo siku ya Jumamosi tarehe 14/05/2016 katika Shule ya msingi Sazira. Katika Mkutano Mkuu huu viongozi wapya wa shirika la BUFADESO wataoongoza shirika kwa miaka mitatu ijayo wamechaguliwa. Vingozi waliochaguliwa kuongoza shirika ni Edward Chacha kutoka kata ya Mcharo- MWENYEKITI WA SHIRIKA, Anifa Malegesi kutoka Neruma - MAKAMU MWENYEKITI, Joseph Itoka wa kata ya Wariku - KATIBU MKUU, Juma Salumu kutoka kata ya GuTA - KATIBU MSAIDIZI na Marwa Nyamhanga - MHAZINI WA SHIRIKA.


Alhamisi, 5 Mei 2016

WAWEZESHAJI JAMII

Shirika la BUNDA FARMER`S DEVELOPMENT SUPPORT ORGANIZATION (BUFADESO) linalenga kufanikisha utekelezaji wa miradi na shughuli endelevu. Ili kufanikisha uendelevu wa shughuli za shirika na miradi ya walengwa yaani jamii, BUFADESO inatumia WAWEZESHAJI JAMII kufundisha, kuelekeza, Kuunganisha na kuwezesha wanachama wa shirika na jamii kwa ujumla.
Wawezeshaji Jamii wa BUFADESO wakiwa na Mratibu wa Shirika Ndg. Baraka Kamese

WAWEZESHAJI JAMII wa shirika la BUFADESO ni wakulima na wafugaji wataalam ambao ni wanachama wa shirika. Wawezeshaji Jamii hawa wamejengewa uwezo na Shirika la Vi AGROFORESTRY na kuhitimu mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo mafunzo ya Uimarishaji wa vikundi, Kilimo na Mabadiriko ya Tabia Nchi, Kilimo Biashara na Ujasiliamali na Masuala Mtambuka kama Usawa wa kijinsia na Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.

Wawezeshaji jamii wa shirika la BUFADESO wanafanya kazi kwa kujitolea katika kata na vijiji wanavyotoka. Kila kata mwanachama wa Shirika la Bufadeso ina wawezeshaji jamii wawili; mwanaume na mwanamke.
Afisa kutoka Vi AGROFORESTRY Bw. Paschal Paul akitoa somo kwa wawezeshaji jamii wa shirika la BUFADESO

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO