Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ShughuliNaMiradi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ShughuliNaMiradi. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 17 Septemba 2019

Serikali, wadau kupunguza athari tabianchi

SERIKALI na wadau mbalimbali wameshauriwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi inayoendelea kuongezeka siku hadi siku nchini na duniani kote.

Hayo yalisemwa na Shirika la Maendeleo la Sweden linalopambana na umasikini na kuboresha mazingira (Vi Agroforestry),  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mara iliyofanyika juzi, yakilenga kukuza uelewa kuhusu mfumo wa ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Masaai Mara nchini Kenya.


Taarifa ya shirika hilo iliyotolewa kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa kutokana na Mto Mara ambao ni muhimu kwa ikolojia ya hifadhi hizo kuwa hatarini kukauka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, suala la uhifadhi wa mazingira halipaswi kupuuzwa.
Ilielezwa kuwa tukio la mwaka huu limewakutanisha wadau kutoka serikalini na mashirika mbalimbali ya uhifadhi kwa kujadili na kukubaliana kuhusu suluhisho litakalosaidia utunzaji wa ikolojia katika hifadhi hizo ambapo kaulimbiu ilikuwa “Mimi, Mto Mara – Simama na mimi/Mimi, Mto Mara – Nitunze nikutunze”.
“Ikolojia na Mara-Serengeti imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi zinazotishia usimamizi wa rasilimali za asili na anuwai ya uhifadhi wa mazingira.
“Changamoto hizi ni pamoja na uchumi jamii, mazingira, athari za mabadiliko ya tabianchi na sera duni, majibu ya kisheria na mwitikio wa taasisi.
“Jamii inayoishi karibu na mfumo wa ikolojia wa Serengeti kwa muda mrefu imekuwa ikikumbwa na migogoro ya wanyama wa porini. Wengi wamekufa na kupoteza wapendwa wao na mazao yao yameharibiwa, simulizi zao zilitufanya kuchukua hatua, kupitia mradi uliofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya unaofahamika kama ‘Sema’,”  ilieleza tarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa mradi wa Sema ni mpango wa uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti, unaolenga kusaidia utunzaji wa mazingira kwa kuziwezesha jamii za watu kuishi maisha endelevu na kuongeza ushirikiano wa kikanda.
Mradi huo unatekelezwa katika maeneo yanayoonekana kuwa na kiwango kikubwa cha umasikini na migogoro kati ya wananchi na wanyamapori.
 “Kwa kushirikiana na Serikali tumeendeleza mpango wa matumizi ya ardhi na mipango ya usimamizi wa chini ya ardhi na sheria ndogondogo za utekelezaji wa shughuli zetu na kutoa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 1,800 kuhusu mipango shirikishi ya utumiaji wa ardhi ili kuanzisha matumizi endelevu ya ardhi.


“Tunaamini panapokuwa miti watu hukua, miti husaidia katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, Kwa hiyo tumeunga mkono jamii kwa kupanda miti zaidi ya 12,000 kando ya Mto Mara na kutoa mafunzo kwa zaidi ya wakulima 2,500 kuhusu kilimo endelevu,” ilieleza taarifa hiyo
Chanzo: Mtanzania Digital

Alhamisi, 16 Mei 2019

Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi


Shirika  la Hifadhi  za  Taifa Tanzania  (TANAPA) kupitia Idara ya  Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa Serengeti linashiriki bega kwa bega katika kutekeleza kazi ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi unaoendeshwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya  Ardhi  (NLUPC)  kwa  kushirikiana  na  Halmashauri  za  wilaya  ya  Bunda na Tarime  na  Vi Agroforestry   Tanzania.   Kazi   hii   ambayo   imelenga   zaidi   kutekelezwa   katika   vijiji vinavyopakana  na  Hifadhi  ya  Taifa  Serengeti  (SENAPA)  pamoja  na  Pori  la  Akiba  la Grumenti  (GGR)  ilianza  kutekelezwa  katika  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Bunda  20 Novemba, 2018 hadi 08 Aprili, 2019 na inaendelea katika wilaya ya Tarime. Malengo ya kazi hiyo ni:
v  Kupunguza/ kuondoa migogoro ya matumizi ya ardhi kati ya vijiji jirani na Hifadhi za Taifa Tanzania ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara
v  Kutoa Elimu ya Uhifadhi, Usimamizi wa rasilimali ardhi na Sheria zinazohusiana na matumizi ya ardhi nchini hususani sheria namba 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999
v  Kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo migogoro ya mipaka na uvamizi wa maeneo ya Hifadhi
v  Kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi na kurejea Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ya vijiji iliyopita muda wake
v  Kumilikisha vipande vya ardhi kwa makundi maalum  ya wananchi wasiojiweza, mathalani wazee, wajane na walemavu
v  Kutoa  mapendekezo  ya  namna  ya  kuboresha  hali  za  maisha  kwa  wananchi kupitia  utekelezaji  wa  miradi  mbalimbali  itakayoibuliwa  wakati  wa  kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji.

Uendeshaji Mafunzo na Uhamasishaji
1. Vikao vya Uhamasishaji wa Viongozi ngazi ya Wilaya
Uhamasishaji kwa viongozi wa ngazi ya Wilaya pamoja na Waheshimiwa Madiwani juu ya Uandaaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji ulifanyika  katika  Halmashauri  zote  mbili  (2)  za  Bunda  Wilaya  na  Bunda  Mji.  Aidha, washiriki wa Uhamasishaji wa zoezi hili walikuwa Mkuu wa Wilaya, Kamati ya ulinzi na usalama,  Wakurugenzi  Watendaji  wa  Halmashauri,  Wakuu  wa  Idara  na  Vitengo  na Waheshimiwa  Madiwani  wa  kata  zinazopakana  na  Hifadhi  ya  Taifa  Serengeti.  Pia uhamasishaji   ulihusisha   Maafisa   Tarafa,   Watendaji   Kata,   Watendaji   wa   vijiji   na Wenyeviti wa vijiji vinavyopakana na SENAPA pamoja na GGR.

2. Mafunzo kwa PLUM za Wilaya
Mafunzo kwa ajili ya Kuzijengea uwezo Mamlaka za Upangaji wa Mipango shirikishi ya Matumizi   ya   Bora   ya   Ardhi   za   Halmashauri   za   Wilaya   (Participatory   Land   Use Management Team -  PLUM) yalifanyika. Timu za PLUM za Halmashauri  ya Wilaya ya Bunda na Halmashauri ya Mji wa Bunda zilijengewa uwezo. Mafunzo yaliyotolewa ni:-
v  Sera, Sheria na miongozo mbalimbali ya uandaaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumzi bora ya ardhi
v  Utayarishaji na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi
v  Matumizi  ya  picha  za  anga  katika  utayarishaji  na  utekelezaji  wa  mipango  ya matumzi ya ardhi ya vijiji
v   Mafunzo  ya  GIS  na  Land  PKS  (kupima  aina  na  uwezo  wa  ardhi  kwa  kuzalisha mazao).

3 Mafunzo kwa Halmashauri za vijiji (VCs), kamati za VLUM na BLAK
 Tangu zoezi hili kuanza mnamo Novemba 20, 2018 hadi kufikia Aprili 04, 2019 jumla ya vijiji 7 vilipatiwa Mafunzo kwa ajili ya kuvijengea uwezo Halmashuri za Vijiji (Mamlaka za Upangaji) na Kamati ya Usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya ardhi ya Vijiji (Village Land Use Management - VLUM) pamoja na Mamlaka za utatuzi wa migogoro ya Ardhi vijijini (Baraza la Ardhi la Kijiji – BLAK) wa kuandaa, kusimamia na kutekeleza mipango ya   matumizi   bora   ya   ardhi   pamoja   na   kutatua   migogoroya   Ardhi   vijijini.   Vijiji vilivyopatiwa  mafunzo  hayo  ni  Hunyari,  Kihumbu,  Mariwanda,  Sarakwa,  Mugeta, Kyandege   na   Tingirima   katika   Halmashauri   Wilaya   ya   Bunda.   Pia   kamati   hizo zimefundishwa sheria mbalimbali za Ardhi ikiwa ni pamoja na:
v  Sera ya Ardhi ya mwaka 1995
v  Sheria ya Ardhi Na 4 ya mwaka 1999
v  Sheria ya Ardhi ya vijiji Na 5 ya mwaka 1999
v  Sheria ya uandaaji wa mipango ya matumizi ya Ardhi Na 6 ya 2007
v  Sheria ya mahakama (utatuzi wa migogoro ya Ardhi) Na 2 ya mwaka 2002
v  Sheria Na. 5 ya Uhifadhi Wanyamapori ya mwaka 2009.

Baadhi ya vijiji ambavyo zoezi hili limefanyika ni;   Hunyari, Kihumbu, Sarakwa, Tingirima, Kyandege,  Mugeta, na Mariwanda katika wilaya ya  Bunda.

Alhamisi, 11 Januari 2018

MAZAO YA BIASHARA YANAYOHAMASISHWA NA SERIKALI

Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu ya biashara yapatayo matano. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo mnamo tarehe 8 Februari 2018 Bungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu. Mazao hayo ya biashara yanayohamasishwa na serikali ni pamoja na Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai.

"Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu. Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.


Mkoa wa Mara umejikita katika kulima zao la Pamba ambalo ndio limekuwa zao la biashara kwa muda mrefu pamoja na changamoto zilizokuwa zinakabili kilimo cha zao hilo hapo nyuma zikiwemo changamoto za pembejeo na bei yenye tija. Katika msimu huu wa kilimo, kutokana na mikakati ya serikali, wananchi wengi wamehamasika kulima zao hili. Shirika la BUFADESO nalo limeandaa shamba la mfano lenye ukubwa wa ekari mbili lililoko kijiji cha Kunzugu, Kata ya Kunzugu wilayani Bunda. Pia wanachama wa shirika wamelima mashamba ya pamba binafsi kuanzia ekari moja na kuendelea.
                                                                                       Shamba la Mfano lililolimwa na shirika la BUFADESO



Jumamosi, 30 Desemba 2017

                                                       
Angalia kipindi cha Jarida Maridhawa la Star Tv kilichoandaliwa na Shirika la BUFADESO kupitia mradi wa uhamasishaji wa Usawa wa Jinsia kupitia Nyimbo na Ngoma za Kitamaduni/Kikabila/Kwaya. 

Jumapili, 24 Septemba 2017

UZINDUZI MRADI WA KUHAMASISHA JINSIA KUPITIA NYIMBO ZA ASILI TAR 22/9/2017


 BUFADESO inatekeleza mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu usawa wa jinsia, ambapo wanachama vikundi walipewa fursa ya Kuandaa Nyimbo zenye ujumbe unao hamasisha usawa wa jinsia na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na mabinti kuanzia ngazi ya familia hadi katika jamii. Ni wazi kuwa jamii yetu ya wilaya ya Bunda inakabiliwa na changamoto ya vitendo vya unyanyasaji wa jinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike. Aidha kutoka na Utamaduni na mila za Makabila mengi ya Mkoa wa Mara, jinsia ya kike imekuwa ikinyanyasika kutokana na matendo kandamizi kama kukeketwa, vipigo kwa wake katika familia, matusi na masimango, watoto wa kike kutopewa kipaumblele cha kupelekwa shule, na kuozwa katika umri mdogo, kunyimwa fursa za umiliki wa rasilimali kama ardhi na mashamba, umiliki wa mali kama nyumba na mifugo mikubwa ikiwemo ng`ombe, wanawake wajane kunyimwa mirathi baada ya waume zao Kufariki na matendo mengine ya kumnyima haki mwanamke kama ushiriki wa masuala mbalimbali ya kijamii. Matendo mengine wanayofanyiwa wanawake yana hatarisha afya zao na muda mwingine hupelekea wanawake kuumizwa, kupewa majeraha au ulemavu na wakati mwingine kusababisha vifo kwa wanawake na kitendo ambacho kinaharibu taifa cha kuwapa watoto wa shule mimba.
Wadau mbalimbali wakifatilia ujumbe uliotolewa katika shughuli ya uhamasishaji wa mradi wa uswa wa jinsia.

Kwa kutambua harakati za serikali katika kushughulikia kumaliza changamoto hii inayokabili jamii zetu ya kutokuwa na usawa wa jinsia na unyanyasaji wa wanawake na wasichana, shirika letu linaunga mkono mapambano hayo na kukemea vitendo vyote vinavyohusiana na kumdhalilisha mwanamke.

Maafisa wa idara za Halmashauri za Wilaya na Mji Bunda kstiks uzinduzi huo

Tunaamini burudani ni njia mojawapo ya kufikishwa ujumbe katika jamii, hivyo kupitia burudani BUFADESO imeona fursa ya Kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya Usawa wa jinsia na kupinga ukatili wa jinsia. Tunaamini kupitia mradi huu unao zinduliwa leo, jamii itapata fursa sio tu kuburudika kupitia burudani zilizo andaliwa bali kupata ujumbe na mwisho wa siku kubadirika na kuacha matendo yanayokiuka utu wa mwanamke. Vikundi wanachama wa BUFADESO vimeandaa Nyimbo na ngoma za kiutamaduni au kikabila zenye ujumbe nzuri unaohamasisha usawa wa jinsia. Nyimbo hizo zinajumuisha Nyimbo za kabila la Wakurya maarufu kama Litungu. Nyimbo za kabila la Waikizu zijulikanazo kama Ndono, Kesa na Bwenga. Nyimbo za Wasukuma Masaligula na Kadumu pamoja na kwaya zenye maudhui ya usawa wa jinsia.
Baada ya Uzinduzi huu, BUFADESO itazunguka katika kata 11 za wilaya ya Bunda tunapofanyia kazi ili kuendeleza kuhamasisha jamii juu ya Usawa wa Jinsia. Pamoja na kuzunguka katika maeneo hayo tofauti, tunaomba ushirikiano wa vyombo vya habari katika kutumia Nyimbo na ngoma hizi zilizo andaliwa ili kuhamasisha jamii juu ya jambo hili. Pia tunaomba serikali iendelee kutia mkazo na kutumia sheria juu ya wananchi wanaoendeleza matendo ya unyanyasaji wa jinsia. Mbali na hayo tuna waasa Wanajamii kutoa taarifa kwenye vyombo husika pale wanapofanyiwa au kuona mwananchi anafanya matendo ya unyanyasaji wa jinsia.

Mwisho kabisa tunaomba na kutoa hamasa kwa jamii hasa watu waliopo vijiji tofauti vya wilaya hii ya Bunda kuacha matendo yote yanayo husiana na kunyanyasa na kukandamiza wanawake na hivyo kusababisha wilaya yetu na mkoa wa Mara kwa ujumla kuwa maarufu kwa sifa mbaya ya Unyanyasaji wa Wanawake. BUFADESO tunaamini kuwa katika familia na jamii yoyote haiwezi kupata maendeleo endapo hakuna ushiriki wa wanawake. Bila ushiriki wa wanawake kuanzia ngazi ya familia shughuli hazitafanyika kwa weledi. Wakulima hawawezi kunufaika na kilimo iwapo mwanamke hapewi fursa ya kushiriki katika shughuli za kutoa maamuzi na mawazo ya kuendeleza kilimo cha familia, hiyo pia haiwezekani katika shughuli za kibiashara, hata katika nyanja ya uongozi; haiwezekani kuwa na ufanisi endapo mwanamke atanyimwa fursa na haki zote anazo stahiki. 

Akizindua mradi huu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili ameilezea jamii kuwa yeye ni mdau mkubwa wa kupinga ukatili wa jinsia. Aidha aliwaasa wananchi kuachana na "mambo ya kale" ya kunyanyasana kwani ni mambo yaliyopitwa na wakati na husababisha kudolola kwa uchumi. Mkuu huyo wa wilaya aliwasisitiza wanacnhi kuachana na mfumo dume na kufanya kazi kwa pamoja. Zaidi aligusia pande zote kuwa wanaonyanyaswa kijinsia sio tu wanawake bali pia wapo wanaume wanaoyanyasika kijinsia na wake zao. Mkuu wa wilaya hii ya Bunda alilipongeza shirika la BUFADESO kwa utekelezaji mzuri wa shughuli zake ikiwemo ya kuhamasisha jamii juu ya usawa wa jinsia.
Mkuu wa wilaya Mwl. Lydia Bupilipili akiongea katika uzinduzi wa mradi wa jinsia, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bunda, Bw. Isaack M. Kabugu na kulia kwake Mwenyekiti wa BUFADESO Edward Chacha
Mwl Lydia aligusa zaidi juu ya shughuli za kilimo kwa wanajamii wa wilaya ya Bunda kwani uchumi wa wilaya hii unategemea zaidi kilimo hasa zao la zao. Mkuu huyu wa wilaya aliwaasa wakulima kurudi kulienzi zao la pamba kwani serikali imeweka mpango mzuri wa kuhakikisha wakulima wanalima kwa tija na kunufaika na kilimo cha zao hilo. aliongezea kuwa serikali imeweka mikakati imara ya zao hilo kuanzia pembejeo hadi mauzo.
Mkuu wa wilaya na viongozi wa BUFADESO wakifurahia burudani na ujumbe kutoka ngoma za kikabila

Alhamisi, 31 Machi 2016

MAFUNZO



Shughuli kubwa ya shirika la Bufadeso ni kuwajengea uwezo wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kuwapa mafunzo na elimu.

Jumanne, 8 Desemba 2015

Vi AGROFORESTRY yakabidhi shughuli kwa BUFADESO

Mradi wa Vi AGROFORESTRY Kanda ya BUNDA ulioanza rasmi mnamo mwaka 2008 katika ngazi ya vijiji vya tarafa ya Serengeti na Chamuriho. Kata 13 ziliwezeshwa kwa kujengewa uwezo wa mafunzo ya mazingira, kilimo, ujasiriamali, uimarishaji wa vikundi na masuala mtambuka ikiwemo usawa na Jinsia na mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.
Mwaka 2009 Vi AGROFORESTRY ilibadirisha mfumo wa utendaji toka ngazi za vijiji kwenda ngazi ya kata.
Mbinu zilizotumiwa ni pamoja na

  1. Kutembelea mkulima mmoja mmoja
  2. Kutoa mafunzo mbalimbali kupitia vikundi vya wakulima.
  3. Kutoa elimu kupitia taasisi hasa mashule
  4. kufanya kampeni za uhamasishaji hasa utunzaji wa mazingira
  5. mikutano na hadhara
  6. mashamba darasa.
Shughuli zikitekelezwa na shirika la VI AGROFORESTRY ni pamoja na:-
  • Ujengaji uwezo kwa kuhamasisha uanzishaji, uimarishaji na uendeshwaji wa vikundi ambapo vikundi 437 vilianzishwa.
  • uhamasishaji juu ya matumizi ya mfumo wa kilimo mseto kwa wakulima.
  • Elimu ya mabadiriko ya tabia nchi.
  • ujasiriamali
  • ushawishi na utetezi
  • masuala mtambuka: masuala ya usawa wa kijinsia, UKIMWI na virusi vya Ukimwi
Tarehe 7 Disemba 2015, Shirika la Vi Agroforestry lilifanya mkutano na wadau ikiwemo serikali na kutangazakuwa kuanzia mwaka 2016, shughuli zilizokuwa zinafanywa na shirika la Vi zitakabidhiwa kwa shirika la Wakulima lililoanzishwa na vikundi vya wakulima, wafugaji na wavuvi wilayani Bunda, BUFADESO. Katika mkutano huo, shirika la Vi AGROFORESTRY lilitoa vyeti kwa wawezeshaji jamii wa BUFADESO waliopatiwa na kufuzu mafunzo mbalimbali.
Meneja wa Vi na Mkuu wa kitengo cha Ujengaji wa Ubia katika mkutano

Mtaalamu wa Vi akisoma ripoti ya utekelezaji wa shughuli

Baadhi ya washiriki katika mkutano

Mwenyekiti wa BUFADESO akitoa maelezo

Muwezeshaji Jamii akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo kutoka Vi AGROFORESTRY

Muwezeshaji Jamii akipokea cheti


Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO