Jumatatu, 18 Julai 2016

SIFA ZA MASHIRIKA YA WAKULIMA NA WAFUGAJI


Kila shirika la kiukulima tunalikumbusha kusimamia misingi mikuu ya shirika ili kuweza kutoa huduma nzuri na zenye tija kwa wanachama wake.Miongoni mwa misingi hiyo ni pamoja na

  1. Shirika lisijihusishe na siasa au dini.
  2. Shirika lisiwe na ubaguzi / ubinafsi katika vikundi vilivyopo katika kata na vijiji.
  3. Shirika  liwe linafanya shughuli zake katika kata husika na vijiji husika kwa mujibu wa usajili.
  4. Shirika liwe linashughulika  na vikundi vya wakulima na wafugaji na siyo vinginevyo.
  5. Shirika liwe na shughuli zinazo onekana na kupimika na zisiwe za kutegesha 
  6. Shirika liwe na uongozi imara unaofata misingi ya utawala wa kanuni na sheria za shirika na nchi, usio na harufu ya rushwa.
  7. Shirika liwe na miongozo inayotafsiri zana ya usimamizi na mifumo ya shirika
  8. Shirike lijikite kusimamia DIRA, DHAMIRA na MALENGO YAKE.
                                

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO