Alhamisi, 15 Julai 2021

FAIDA ZA VIKUNDI VYA KIJAMII VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

 BUFADESO kupitia mradi wa ALIVE imekua ikifanya uhamasishaji wa mifumo ya kifedha vijijini (kuweka na kukopa) Hisa kupitia vikundi vya kijamii vya Huduma Ndogo za Fehda. Kupitia program hii watu mbalimbali wamekua wakinufaika hasa wanawake, Pichani ni Mama, Miriam Samsoni 55, Mama huyu ameweza kuweka umeme na kujenga nyumba kupitia fedha alizopata baada ya kumaliza mzunguko wa Hisa Mwanzoni mwa mwaka huu 2021 sio hivyo tu Bali amekua akisomesha watoto kupitia fedha anazokopa kwa riba nafuu kupitia kikundi chake Cha Kijamii cha Huduma Ndogo za Kifedha cha Umoja kinachopatika kata ya Sazira, Bunda.

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO