KAMATI YA UCHAGUZI ya shirika la BUFADESO inapenda kuwatangazia wanachama vikundi vya shirika kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la BUFADESO utafanyika kati ya tarehe 13 hadi 16 Disemba 2022. Uchaguzi huo utajumuisha Nafasi zifuatazo:
1) Mwenyekiti wa Shirika
(Nafasi moja)
2)
Katibu wa Shirika (Nafasi moja)
3)
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi (Nafasi saba)
BUFADESO inawatangazia wajumbe wote wa vikundi
wanachama na wanachama binafsi wenye sifa na weledi wa kujaza nafasi hizo
kutuma maombi ya kugombea nafasi hizo.
SIFA ZA MWOMBAJI:
1.
Awe
mwanakikundi wa kikundi mwanachama hai wa shirika la BUFADESO au mwanachama
binafsi wa shirika.
2.
Ajue
kusoma na kuandika.
3.
Asiwe
muajiriwa wa serikali.
4.
Awe
mbunifu mwenye ari ya maendeleo.
5.
Awe
mwaminifu na muadilifu.
6.
Awe
anayekubali mabadiliko anapopewa changamoto mbalimbali.
Mwanakikundi
mwenye sifa tajwa na mwenye mwamko wa kuongoza atume barua ya maombi
ikiambatana na fomu ya maombi ya kugombea
nafasi ya Uongozi iliyojazwa kwa usahihi, inayopatikana kwa watumishi, wawezeshaji
jamii, na viongozi wa vikundi:- Fomu hii italipiwa baada ya kutuma maombi kiasi
cha Tsh 10,000/- (elfu kumi tu) kupitia akaunti ya
shirika benki ya NMB yenye jina la MTANDAO WA WAKULIMA BUNDA namba 30110004259.
(Wanawake na vijana wanahamasishwa
kugombea nafasi hizo)
Maombi
yatumwe kwa;
Kamati
ya Uchaguzi,
BUFADESO,
S.L.P.95,
BUNDA
Mwombaji
atume maombi kwa sanduku la posta lililotajwa hapo juu au umpe mwezeshaji jamii
au mtumishi wa BUFADESO au afikishe maombi yake katika Ofisi za BUFADESO
zilizopo Sazira.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/11/2022
saa kumi na moja jioni.
Imetolewa na
KAMATI YA UCHAGUZI
BUFADESO