Jumanne, 24 Novemba 2015

Shirika la Wakulima

Shirika la BUFADESO linatoa huduma ya kuwajengea uwezo wanachama wake kwa kuwaelimisha masuala yanayohusu kilimo, ufugaji, uvuvi,  utunzanji wa mazingira na makabiliano dhidi ya mabadirikio ya tabia nchi, ujasiliamali na kilimo mseto & kilimo biashara.
Mwezeshaji jamii wa shirika la BUFADESO akitoa maelezo katika mafunzo

BUFADESO ni shirika la wakulima na wafugaji linaliundwa na vikundi. Miongoni mwa vikundi hivi ni pamoja na
1. Vikundi vya kuweka na kukopa.
2.Vikundi vya wanawake(kina mama)
3.Vikundi vya vijana
3.Vikundi vya ufugaji
4.Vikundi vya kilimo
5.Vikundi vya upandaji miti
6.Vikundi vya kusaidiana
7.Vikundi vya wajasiriamali
8.Vikundi vya Kujifunza

Jumamosi, 14 Novemba 2015

MAELEZO MAFUPI KUHUSU BUFADESO

TAREHE YA KUANZISHWA KWA SHIRIKA:
Shirika la BUFADESO lilianzishwa Tarehe 27/02/2012

USAJILI:                                                                                                                                          
Shirika limesajiliwa mnamo tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696 chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya kiserikali. 
DIRA YA SHIRIKA:                                                                                                                         
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda
DHAMIRA YA SHIRIKA:                                                                                                       
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu
LENGO KUU:                                                                                                                                
 Kuwa na wakulima wanaotumia na kunufaika na mbinu bora za kilimo ifikapo 2025
MALENGO MADOGO MADOGO:
1)      Kuwa na wakulima wanaotumia mbinu bora za kilimo ifikapo 2018
2)      Ongezeko la kaya za wakulima na wafugaji wanaotumia mbinu za kilimo bora ifikapo 2017
3)      Uwepo wa wakulima na wafugaji wanaojishughulisha na kunufaika na kilimo biashara ifikapo 2018.
4)      Kuwa na wakulima wanaohifadhi mazingira na wanaoweza kukabiliana na athari za       mabadiriko ya hali ya hewa ifikapo 2019
5)      Kuwa na vikundi vyenye shughuli na miradi endelevu ifikapo 2017.

SHUGHULI ZA SHIRIKA:
   i.            Kutoa Elimu na mafunzo kwa wanachama
    ii.            Kuratibu shughuli za wanachama wa shirika.
  iii.     Ushawishi na utetezi katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kimazingira ili kuleta maendeleo endelevu kwa jamii na wanachama
    iv.            Kuwakilisha wanachama kwenye ngazi za juu.
     v.            Kuhamasisha masuala mtambuka hasa UKIMWI/VVU na usawa wa kijinsia.

MAADILI YA SHIRIKA:
Utendaji kazi utajikita katika viwango vifuatavyo:-
                                i.            Uaminifu.
                              ii.            Heshima na kuthaminiana.
                            iii.            Ushirikiano.
                             iv.            Kuzingatia na kujali muda.
                               v.            Kutozingatia ubaguzi wa aina yoyote    
                             vi.            Kudhibiti rushwa.         


                                           

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO