Jumanne, 15 Oktoba 2019

SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Leo ni SIKU YA CHAKULA DUNIANI. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa” :kauli mbiu
hii inalenga kuhamasisha jamii na wadau wote wa sekta kilimo kuchangia katika
kuhakikisha nchi na dunia inakuwa na chakula cha kutosha wakati wote.

Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonyesha hali ya
upatikanaji chakula mwaka 2019/2020 ni nzuri, kwani nchi, ina chakula cha
kutosha. Kiwango cha utoshelevu wa chakula ni asilimia 119. Uzalishaji wa mazao
ya chakula ulifikia tani 16,408,309 ukilinganisha na mahitaji ambayo ni
tani  13,842,536. Kati ya hizo Tani
9,007,909 ni mazao ya nafaka na tani 7,400,400 ni mazao yasiyo
nafaka.
Tunawapongeza wadau wote wa sekta ya kilimo wanaoendelea kuhakikisha sekta hii inapunguza changamoto zinazowakabili wakulima
#WorldFoodDay
#SikuYaChakulaDuniani

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO