Ijumaa, 29 Januari 2016

MABADILIKO YA TABIA NCHI

 Mabadiliko  ya  tabia  nchi  ni  mabadiliko  yanayojitokeza kwa  muda  mrefu  kama  vile  joto,mvua nyingi  au  chache ,ukame,  kuongezeka  kwa  hewa  chafu  (hewa  ya  ukaa)  angani.
Hali  hii  inasababisha  uasilia  wa  vitu  vilivyokuwepo  kuharibika  au  kupotea  kabisa

VISABABISHI
Chanzo kikubwa cha mabadiriko yatabia nchi kimesababishwa na shughuli za binadamu kutokana na:
-Ongezeko  la  binadamu(watu)
-Uelewa  mdogo  (uhalibifu  wa  ardhi  na  uhalibifu  wa  misitu)
-Ufugaji  holela 
-Uchomaji  moto  ovyo 
Ongezeko  la viwanda- na  hili  linachangia  zaidi.
Pamoja na  mafuta  mazito  ambayo  yakiungua  hutoa  kiasi  kikubw  cha  hewa  ya  ukaa(co2)



SABABU  ZA  UHARIBIFU  WA MAZINGIRA
-Hii  husababishwa  na  shughuli  za  kimaendeleo  anazozifanya  binadamu  kama  vile:-
-Ukataji  wa  miti  katika  upanuzi  wa  mashamba.
-Uchomaji  wa mkaa
-Biashara  ya magogo
-Ukusanyaji  wa  kuni(matumizi  makubwa  ya  kuni)
-Shughuli  za  migodi  ya madini 
-Ukataji miti ovyo-mbao
-Uchomaji  moto ovyo
-Mifugo  mingi  katika  eneo  dogo
-Ukuaji  wa  miundo  mbinu  na  ongezeko  la viwanda  ,mitambo   pamoja  na  vyombo  vya  usafiri  vinavyotumia  dizel
-Kilimo  kisichozingatia  mbinu  bora  za  lilimo

Kutokana  na  mabadiliko  hayo,  matumizi  haya  yakiendelea/yanapoendelea  yanapelekea:-

Ø  Kuzolota  kwa  kilimo  (uzalishaji  hafifu)  kushamili  kwa  umaskini
Ø  Milipuko  ya magonjwa 
Ø  Kutokea  kw  dhoruba  kali  ya  upepo  na  kusababisha  uharibifu  wa mazao  na  kuezuriwa  kwa  nyumba  /makazi  ya watu  wakati  mwingine  hata vifo  visivyo tarajiwa(vya  ghafla).
Ø  Ukame
Ø  Barafu
Ø  Tetemeko  la ardhi  n.k


Ardhi-sasa hivi  ardhi  yetu   imepoteza  rutuba/ imechoka  ,kile  unacho  kusudia  kukipata  hakipatikani hii    ni   kutokana  na  kupanda  mazao  kwa  muda  mrefu  bila  kuongeza  mbolea. Pia  na  kutumia  mbolea  za  viwandani  zinahalibu  ardhi  yetu  kwani  muda  /siku  ambayo  utakosa  mtaji  wa  kununua  mbolea  hizo,   muda/siku  ukipanda  mazao  bila  kuweka  mbolea  hizo  za  viwandani  hutaweza  kuzalisha  chochote.Vilevile  mbolea  za  viwandani  na  madawa  ya  viwandani  yakitumika  yanaua wadudu  rafiki  walioko  udongoni  wanao  saidia  kumengenya  mbolea au maozea na  kusababisha  ardhi  isiweze  kupumua vizuri  (mzunguko  hafifu  wa  hewa  ardhini).

Misitu- Uhalibifu  wa  misitu/ukataji  miti  holela  unasababisha  uhalibifu  wa  mazingira.(ardhi)

Mifugo- Mifugo  inayoogeshwa  dwa  zizini  bila  kutumia  crash,  ile  dawa  ikimwagika kudondoka  kwenye  mbolea  inaua  na  kuhalibu  wadudu  walioko  kwenye  mbolea  .Hivyo  mbolea  hiyo  ikitumika  kupandia  mazao  haifanyi  vizuri  kwani  ile  dawa(sumu)  inakuwa imeua  na  kuharibu  wale  wadudu  ambao  wangesaidia  kumengenya  vizuri  ile mbolea  na mzunguko  wa  hewa  ardhini  kwenda  kwa  utaratibu  mzuri 

Ili  tuweze  kujinusuru  na  hali  hii  yatupasa  kutumia /kuchukua   hatua  kuu  3  nazo  ni -1.Kusikia.  2.Kuamini.  3.Kufanya  maamuzi.
KIla mmoja  akifuata  hatua  hizi  tatu  tunaweza  kuondokana  na hali  ngumu  ya mabadiliko  ya tabia nchi   inayo  tuletea /pelekea  UMASKINI  wakati  muda  wote  /mwingi  tunaonekana  tunafanya  kazi  za  uzalishaji  lakini  tunachokizalisha  hakilingani  na  nguvu  zetu.

MASWALI  YAKUJIULIZA

*Tufanye    nini  ili  kuondokana  na  hali  hii  ya uhalibifu  wa  mazingira
*Ni  mbinu  zipi  tuanze  kuzitumia  katika  eneo  letu  ili  zilete  ufanisi
*Tuanze  lini  shughuli  hizi.
*Nimsaada  gani  tupate  toka  kwa  wataalam
Nimahitali  gani  yanahitajika ili  kufanikisha  shughuli  hii.
Nini  kifanyike


Ili  kupunguza  makali  haya  na  sio  kuzuia kabisa  lazima tutumie  mbinu  endelevu  za  matumizi  ya  ardhi  ya  kilimo  na mbinu  hizi  endelevu  zitaegemea  zaidi  katika  kukabiliana  na mabadiliko  ya tabia  nchi  katika haya  yafuatayo:-
*Mabadiliko  ya  hali  ya  hewa(kuongezeka  kwa  gesi  joto),  mabadiliko  makubwa ya vipindi  vya  mvua ,ukame  barafu  na mafuriko.
*Uzalishaji  mdogo  wa mazao
 *Rutuba  ya udongo(afya  ya udongo)
*Wadudu na magonjwa
*Vyanzo vya maji
*Nishati mbadala  eg  mwanga  wa  jua  na  Biogesi
*Chakula na lishe.


MBINU  ZITAKAZOTUMIKA
·         Kilimo mseto-kilimo  mchanganyiko  wa  mazao,  miti  na mifugo 
·         Kilimo  cha vijishamba  vya miti
·         Matandazo-
·         Kilimo  mzunguko(mzunguko  wa mazao)
·         Mifumo  rahisi  ya uvunaji  wa  maji  ya  mvua 
·         Matumizi  ya mbolea  itokanayo  na mifugo,,mbolea  za asili (mbolea  vunde)
·         Mazao  funika 
·         Kilimo  hifadhi(kilimo  cha   kutotifua  au  kutifua  kwa  kiasi  kidogo.
·         Matumizi  ya  dawa  za  asili
·         Ufugaji  wa  ndani (ufubaji  unao  kidhi)
·         Ufugaji  wa  Nyuki  na  ufugaji  wa  Samaki  kwenye  mabwawa
·         Kupanda  mazao  katika  kontua(contour)
·         Terrace
·         Matumizi  ya mimea  (miti)  ya asili  inayohimili  ukame 
·         Mazao  yaliyo  boreshwa  yenye  uwezo  wakuhimili  wadudu  na magonjwa(mazao  kinzani)
·         Umwagiliaji
·         Utumiaji  wa  majiko  sanifu/banifu
·         Uzalishaji  wa mkaa
·         Urutubishaji  wa  udongo  kwa  kutumia  mabaki /masalia ya  mazao  mf   mabua  ya Mahindi,Ngano,Mtama,Viazi  n.k
·         Kutumia  mbolea  za  kijani
·         Palizi  kwa  wakati  muafaka.


Mkulima  akitumia mbinu  hizi  hakika  ataweza
v  Kukabiliana  na mabadiliko  ya  tabia nchi
v  Mata asili  na matokeo  yake  mavuno  yataongezeka
v  Ataondokana  na utegemezi  wa mbolea  na  madawa  ya viwandani
v  Kuongezeka  kwa  viumbe  hai   katika  udongo
v  Kuondoa  gesi  ya  ukaa  hewani/angani 
v  Atapata  faida  ya  ziada  -   mbao  na  kuni.
v  Atapata  soko  zuri  la  mazao (bithaa  bora)
v  Kipato  kitaongezaka  (mkulima  atajikwamua  na  hali  ngumu  ya  maisha(umaskini)
v  Nazaidi  itasaidia  kulinda/kutunza  chakula  kwa  kizazi  kijacho  (usalama  wa  chakula)

Njia  kuu  tano  za  kufanikisha  mbinu  endelevu  za  matumizi  ya  ardhi  ya  kilimo  ni-
1)      Uzalishaji  wa mazao  kwa  wingi  na  ubora
2)      Utunzaji  wa  mazao
3)      Utunzaji  wa  mifugo
4)      Ufanisi  wa  nguvu  na  matumizi  ya  bio-gas  na  nguvu  za  jua  (solar)
5)      Uanzishaji  wa  vitalu  vya  miti
6)      Upandaji  na  utunzaji  wa  miti


Matandazo  na  faida  zake (mulching)
   Matandazo  -  Niufunikaji  wa  udongo  kwa  kutumia  mabaki  ya mazao  au  majani.Yaweza  kutumiwa  shambani  kabla  au  baada  ya  upandaji,pia  na  kando  kando  ya  mimea  ili  kufunika  udongo.Matandazo  kwa  wastani  ni  mazuri  kwenye  sehemu  kavu  na  wakati  wa  misimu  kavu,  hata  wakati  wa mvua  ili  kuzuia  mmomonyoko  wa  udongo.
-Huongeza  mbolea(mata  asili  kwenye  udongo)
-Hutunza  joto  kwenye  udongo
-Hutunza  unyevunyevu
-Huifadhi  viumbe  hai
-Huzuia  magugu  kuota
-Huzuia  upotevu  wa  maji
-Hufanya  shamba  kuwa  safi(muonekano  wa  shamba)


Kilimo  mseto:-
Ni  kilimo  chamchanganyiko  wa  miti  na  mazao  shambani yaliyopandwa  kwa  nafasi  maalum  kitaalam  ya  muda  mrefu  na muda  mfupi  pamoja  na mifugo  katika  eneo  moja  la  shamba.
Ø  Kilimo  mseto    kina  uwezo  wa  kustawi  kwenye    udongo  usio  na  rutuba  ,kina  mizizi  ambayo  huenda  chini   na  inauwezo  wa  kufikia  virutubisho  kutola  kwenye   tabaka  la  chini   la  udongo  bila  kushindana  na mazao  mengine   yaliyopandwa  shambani
Ø  Virutubisho  kwenye  majani  ya  miti  huanguka  chini  na  kuvunda  nakuongeza  matahuruku  kwenye  udongo.
Ø  Husaidia  kupata  mazao  mbalimbali  kama  vile  matunda, mbogamboga,chakula,mbolea  za asili, samadi, mbao  na  kuni, dawa  na  mengineyo.
Ø   Hushikamanisha  udongo na  kuzuia  mmomonyoko  wa udongo
Ø   Huifadhi  mazingira.

Mazao  funika (cover  crops)
Ni  mazao  yanayopandwa  kwa  ajili  yakufunika  ardhi   kama  vile  Mucuna,Lablab,Canavalia, Desmodium,Tephrosia, Sesbania   Mbaazi n.k
-Huifadhi  udongo  kwa  sababu  hufunika  ardhi
-Huzuia  mmomonyoko  wa  udongo  .
-Huzuia  magugu
.Huzuia  sura  ya  udongo.
-Huongeza  rutuba  ya  udongo.
-Hutunza  unyevunyevu.
-Huzuia  maji  kutiririkaovyo  na hutunza  maji  yasipotee  hewani.
-Hutupatia  kuni,dawa  nanyingine  malisho  ya  mifugo
-Mengine  hutupatia  chakula  kam  mbaazi


Mbolea  vunde  (compost  manure)
Mbolea  vunde  ni  limbukizo    la mbolea  /takataka / masalia  ya mazao   na  mimea  iliyo  kusanywa  kwenye  mashimo  zikivundwa  /kuoza   zaweza  kutengenezwa  kwa  kutumia  vitu  kama  hivyo  na  kutoa  mbolea  vunde,  na  kutoa virutubisho  kwa  mimea  /Mbolea  vunde    hutengenezwa  kwa  kuozesha  takataka  mbalimbali  kama  vile  magugu  na  maganda  ya mazao  ya  chakula  (ndizi,  maharage,viazi  vitamu  Alizeti  pori   n.k  )   vitu  hivyo  vinachanganywa  na  majivu, nyasi  kavu  kinyesi  cha  mifugo na udongo.  Vitu  vilivyo  vundikwa  vinaweza kuongeza  rutuba  katika  udongo  wa  aina  tofauti.
Uwezo  wa  udongo  kutoa  virutubisho  hupungua  kadri  tunavyoendelea  kustawisha  mazao. Hivyo  ni  lazima  kutumia  juhudi  na  maarifa  ili  kuboresha    na  kudumisha  virutubisho  vya  mimea  kwenye  mashamba  yetu
Nanjia  mojawapo   yakufanya  hivyo nikutengeneza   mbolea  vunde/ mboji.


Faida  ya mbolea  vunde/mboji 
Ø  Gharama  yake  ni  ndogo   kuliko  aina   nyingine  za  mbolea 
Ø  Huboresha /hurutubisha   vizuri  hali  ya  udongo  na  kukaa  muda  mrefu    zaidi  kuliko  mboea  za  viwandani.
Ø  Huboresha  sura  ya  udongo
Ø  Hutengenezwa  kwa  urahisi
Ø  Hutunza  vizuri  viumbe  hai
Ø  Huboresha  mzunguko  mzuri  wa  hewa  kwenye  udongo
Ø  Huchanganyikana  na  udongo  bila  kuachana
Ø  Hurutubisha  mimea  haraka
Ø  Huboresha  ladha  ya  chakula (Bidhaa bora  katika  soko  la Kimataifa  na  soko  letu  kwa  ujumla) na  kulinda  afya  zetu.





Kilimo  mchanganyiko(Intercropping)

Ni  kilimo  kinacholimwa  kwa  kuchanganya  mazao  mawili  au  zaidi  kwa  mistari  katika  eneo  moja  la  shamba /kwa msimu  au  wakati  mmoja
Mbinu  hii husaidia  kuboresha  udongo  ikiwa  umetumia/umepanda  mazao  yanayotoa  mbolea  ardhini  na  yanayoingiza  mbolea  ardhini/udongoni.
Mf  mahindi  na  maharage  karanga  na viazi  vitamu


Mbolea  za  wanyama
Ni  kinyesi  cha  wanyama  ambacho  hukusanywa  kwa  urahisi  kutoka  kwenye  banda (zizi)  ufugaji  wa  ndani  na  kuvundikwa  moja  kwa  moja  kwa  kufunikwa  na  majani/nyasi  kavu  kabla  ya  kusambazwa  shambani  kwa  muda  wa  miezi  mitatu
Wanyama  ambao  hupata  malisho  bora  hutoa  mbolea  yenye  virutubisho  vingi  zaidi  kama  vile  calliandra,Lusina,  Desmodium,  Sesbania n.k
Huboresha  mazao, huunganisha  udongo ,huifadhi  kiasi  cha  maji  kwanye  udongo 
Huongeza  upenyaji  wa  maji  kwenye  undongo


Kontua (contour  and  terrace)

Kontua  ni  mitalu  inayolimwa  /chimbwa  kufuatana  au  kulingana  na  hali  halisi  ya  mteremko  kwa    kutumia  vipimo maalum (A-frame  na  mambo)  na  kuweka  alama  katika  eneo  lenye  mteremko  .  Na  hiyo  A-frame  ni  vema  itumike  wakati  wa  kiangazi  ambapo  ardhi  inakuwa   ngumu/imegandamizwa  hivyo   miguu  ya  A-frame  haididimii  katika  udongo  .
Mtalu  huo  ukisha  chimbwa  au  kulimwa  unasaidia  kuzuia  mmomonyoko  wa  udongo, kuzuia  maji  ili  yasipotee/yasitiririke  haraka  na   nakupoteza  au  kusomba  virutubisho  kutoka    eneo  husika
Hutunza  maji  na  kulishia  shamba  taratibu 
Huzuia  virutubisho  kupotea  toka   eneo  husika



Palizi 
  Ni  tendo   la  kuondoa  magugu  shambani  na  kuweka  mazao  katika  hali  nzuri.
Hupunguza  ushindani  wa  ufyonzaji  wa  virutubisho  na  maji  toka  shambani
Husaidia  kupunguza  wadudu  na  magonjwa  shambani
Hulifanya  shamba  kuwa  na muonekano  mzuri (shamba  kuwa  safi)

Kuna  njia  mbili  za  kuondoa  magugu  shambani-
1.Palizi  kwa  kutumia  jembe  au  mikono
2.Palizi  lakutumia  madawa  ya  viwandani  na njia  hii  sio  nzuri  kwani  ikitumika  inaua  wadudu  marafiki  mashambani.


UTUNZAJI  MAZINGIRA  KWA  KUTUMIA  MAJIKO  SANIFU
Utumiaji  wa  majiko   sanifu  / banifu  kwa  jamii  kwa  lengo  la  kutunza  mazingira.
Majiko  sanifu    lengo  lake  ni  kubana  matumizi  ya  kuni  kwa  kutumia  kuni/mkaa  kidogo  ili  kupunguza  ukataji  miti  ovyo,kuwa  na  uoto  wa  asili  na kuwa  na  misitu  ya  kutosha  katika  jamii  zetu .Pia  kuwa  na  uwezekano  mzuri  wa  kutunza  mazingira   na  kuepukana  na  jangwa   kama  ilivyo  sehemu  nyingine  hapa  nchini  na  Afrika  kwa  ujumla
Elimu  duni   inafanya  jamii  zetu  kuwa  na  uchangiaji  mkubwa  wa  uharibifu  wa  mazingira  hasa  kwa  nchi  yetu  Tanzania.
Kutokana  na   hali  hii  Tanzania  kupitia  mashirika  mbalimbali  na  serikali  kwa  ujumla  imekuwa  imeanzisha  mkakati  mahususi  wa  kutoa  elimu  kwa  jamii  zetu  kuhusu  utunzaji  wa  mazingira.
Kwa  kutumia  mbinu  endelevu  za  kilimo  na  hii  ni  pamoja  na  utengenezaji/utumiaji  wa  majiko  sanifu/banifu  ili  kusaidia  /kujinusuru  na  wimbi  la  umaskini  na  kuwa  wajasiliamali  wazuri  kwa  kutumia rasilimali  tulizo  nazo,  kufanya  mazingira  kuwa    masafi  na  endelevu,  kutunza  raslimali  zilizopo  kwa  ajili  ya  kizazi  kijacho  .
Mazingira  ni  mambo  yote  yaliyomzunguka  binadamu  ambayo  ni  viumbe  hai  na  visivyo  hai



UTENGENEZAJI  WA  MBOLEA  VUNDE

Kuna  njia  mbili  zakutengeneza  mbolea  vunde /mboji
          1.Kutengeneza  kwa  kutumia  mlundo
          2.Kutengeneza  kwa  kutumia  shimo



Njia  zote  mbili    hutumiwa  kwa  kufuatana  nahali  ya  hewa  ya mahali  ulipo.
          -Sehemu  zenye  mvua  nyingi  na  mvua  za  kadri,  tumia  njia  ya  mlundo
          Njia  hii  hupunguza  unyevu    nakulifanya  lundo  liweze  kuoza  vizuri.
          Sehemu  zenye  mvua  kidogo  tumia  njia  ya  shimo.
          Njia  hii  hutunza  unyevu  ili  lundo  liweze  kuoza  vizuri



Hatua  za  utengenezaji  wa  mbolea  vunde/ mboji

§  Tayalisha  vifaa vifuatvyo:-Jembe,vifaa  vyakuchotea  maji,kijiti  chakupimia  joto, nguzo,nyasi/majani, mabua  ya  mahindi,  majivu  samadi  na  udongo
§  Pima  eneo  lenye  urefu  wa  meta  2  na  upana  wa  meta  2 mraba
§  Simika  nguzo  kila  pembe  ya  eneo
§  Jenga  tabaka  lakwanza  la  mabua    makavu /   nyasi  kavu  kama  huna  mabua  ya  mahindi  sentimeta  10-15  unene.
§  Kama  umepata  mabua  juu  ongezea  nyasi  kavu
§  Jenga  tabaka  la  samadi  /kinyesi  cha  mifugo  sm  5  - 10
§  Weka  juu  udongo  kidogo  sm  2
§  Ongeza  tabaka  la  takataka,  masalia    ya  mazao  n.k  hili  ndilo  tabaka  kubwa  sana  kuliko  zote  litakalo  unda  sehemu  kubwa  ya  mbolea,  unene  sm  15.
§  Mwagilia  maji  yakutosha  ili  tabaka  zote  zipate  unyevu  ziweze  kuoza  vizuri.
§  Juu  weka  tabaka  la  majivu  kusaidia  uvundaji/uozaji  wa  tabaka  nyingine  sentimeta  2
§  Jenga  tabaka  la  samadi / kinyesi  cha  mifugo  sm  5-10
§  Fanya  hivyo  kila  baada  ya  tabaka  la  udongo
§  Rudia   mpangilio  huu  kuanzia    na  nyasi  kavu  mpaka  lundo  lifikie  kimo  cha  meta  1.5
§  Baada  ya  kufikia  kimo  hicho  lundo  lifunikwe   kwa  nyasi  au  magunia  au  mikeka  iliyo  chakaa.n.k
§  Juu  kabisa  ya  lundo  jenga  kivuli    ili  mvua  na  jua  visiharibu  ubora  wa  mbolea
§  Lundo  ligeuzwe  kila baada  ya  majuma  matatu  ili  tabaka  zilizo chini  ziwe  juu  na  za  juu  ziwe  chini  kwakuhamishia  eneo  lingine.
§  Kata   kijiti  kirefu  kasha  kichomeke  katikati  ya  lundo,  Hiki  kitakusaidia  kupima  joto    nakuangalia   mbelea  kama  inaendelea  kuoza  vizuri  (unyevunyevu  wakutosha)

Mambo    muhimu  ya  kuzingatia
        *Ujenzi  wa  lundo  ukamilike  kwq  siku  moja  tu
        *Chomoa  kijiti  kila   baada  ya  siku  nne  ili  kupima  joto  la  lundo
        *Iwapo  lundo  halina  joto  la  juu  fahamu  kuwa  halijaoza
        *Ikiwa  uozaji  umekwenda  vizuri  mbolea  itakuwa  tayari  baada  ya  miezi  miwili  hadi  mitatu
        *Tengeneza  mboji/mbolea  vunde    nyingi  kwenye  musimu  wa mvua

Kilimo  mzunguko /  mzunguko  wa  mazao (crop  rotation) 
 Kilimo  mzunguko  ni  kilimo  kizuri  sana    kwani  kinasaidia 
-Kuzuia  wadudu  waharibifu  wa  mazao, magugu  na  magonjwa.
-Pia  kilimo  hiki  husaidia  kuongeza  mbolea  kwenye  udongo  kwani  unapopanda  mazao  yanayotoa mbolea  na  musimu  unaofuata/mwingine  unapanda  mazao  yanayoongeza/ ingiza  mbolea  ardhini   mf  ukipanda  mahindi  na  baadae  musimu  unofuata  unapanda  maharage  au  karanga.

Mbolea  za  kijani (Green  manure )  
-Ni  mimea  au  miche  inayopandwa  kwa  madhumuni  ya  kufunikawa  /kutifuliwa   kwenye  udongo  ili  kuongeza   mbolea /virutubisho  zaidi  kwenye  udongo
-  Ni  mimea  inayopenyeza  / ingiza  Nitrogen  kwenye  udongo (sana sana  mikunde  kunde)
-Mimea  hii  hukua  haraka,hufunika  ardhi (udongo)
-Huzuia  mmomonyoko  wa  udongo
-Mbolea  hii  husaidia  maji  kupenya  kwa  urahisi
-Huzuia  magugu  kuota
-Hupunguza  magonjwa  na nematode
-Nichimbuko  la  malisho  ya  mifugo
-Mimea  mingine  huzalisha  chakula  cha  binadamu
-Haitumii  nguvu  kazi  nyingi
-ni  nzuri  kwa  udongo  usio  na  rutuba  na  mkavu.

TUMIA MBINU  HIZI  KWA  KUTUNZA  MAZINGIRA,  NA  KABILIANA  NA MABADILIKO  YA TABIA  NCHI

 Imeandaliwa na BARAKA KAMESE
                             Mratibu - BUFADESO

Jumatatu, 18 Januari 2016

TUJIUNGE NA VIKUNDI VYA HISA

Vikundi vya Hisa (kuweka na kukopa) ni mpango uliosaidia na unaoendelea kusaidia maisha ya wakulima vijijini kupata fursa ya kujiwekea akiba na kupata mikopo yenye masharti nafuu. Mpango huu umesaidia kuinua maisha ya wakulima hasa kupata mitaji ya kuanzisha na/au kuendeleza shughuli za kilimo na ufugaji pamoja na biashara ndogondogo.
                                                                                 Wanachama wa kikundi cha Hisa kutoka kijiji cha Sarawe wilayani Bunda

Vikundi vya Hisa ni vikundi gani?
Hivi ni vikundi vya kuweka akiba(fedha) na kukopeshana vinavyoundwa kwa hiari na watu wanaojuana kutoka sehemu moja. Wanakikundi hupata fursa ya kuweka akiba, kupata mikopo na kupata fursa ya huduma ndogondogo za kijamii kama afya na elimu. Mikopo katika vikundi hivi hurudishwa na ziada(riba) nafuu. Mwisho wa mwaka wanachama hugawana hisa, riba na faini zilizokusanywa katika mzunguko kulingana na Idadi ya hisa kila mwanachama alizonunua ndani ya mwaka.
Wadau wa vikundi vya hisa mara nyingi ni watu wa jinsia zote, Wanawake na Wanaume. Kikundi kimoja cha Hisa huwa na wastani wa wanakikundi kati ya 15 mpaka 30. Uzoefu unaonyesha kuwa vikundi vyenye wanachama wengi kupita kiasi huwa vina kosa ufanisi wa Uendeshaji hasa pale kikundi kinapokuwa na tabaka la watu wa kawaida. Ni vizuri kikundi cha hisa kiwe na Idadi ya wanachama wasiozidi thelathini (30).
Faida za vikundi vya Hisa ni pamoja na
v  Kusaidia wanachama kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi.
v  Ziada ya mkopo (riba) ni kidogo hivyo haimuumizi mkopaji.
v  Mwanachama hupata gawio la faida inayopatikana.
v  Ni rahisi kuweka akiba kutokana na kiasi kiwango kidogo ambacho wanakikundi hukubaliana kwa pamoja.
v  Huwezesha wanakikundi kupata fursa na huduma za kijamii kama afya na elimu.
v  Ni rahisi kuendesha kikundi.
v  Wanakikundi hupata fursa ya kuelimika katika kikundi.

Shirika la BUFADESO lina wanachama wanaonufaika na mfumo wa Hisa. Asilimia 60 ya wanachama wa shirika wanapata huduma za Mfumo wa Hisa katika vikundi vyao. BUFADESO hutoa elimu ya uandaaji, uanzishaji, uimarishaji wa vikundi vya Hisa kwa maendeleo ya wakulima, wafugaji na wavuvi wa wilaya ya Bunda.

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO