Alhamisi, 11 Januari 2018

MAZAO YA BIASHARA YANAYOHAMASISHWA NA SERIKALI

Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu ya biashara yapatayo matano. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo mnamo tarehe 8 Februari 2018 Bungeni Mjini Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu. Mazao hayo ya biashara yanayohamasishwa na serikali ni pamoja na Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai.

"Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu. Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.


Mkoa wa Mara umejikita katika kulima zao la Pamba ambalo ndio limekuwa zao la biashara kwa muda mrefu pamoja na changamoto zilizokuwa zinakabili kilimo cha zao hilo hapo nyuma zikiwemo changamoto za pembejeo na bei yenye tija. Katika msimu huu wa kilimo, kutokana na mikakati ya serikali, wananchi wengi wamehamasika kulima zao hili. Shirika la BUFADESO nalo limeandaa shamba la mfano lenye ukubwa wa ekari mbili lililoko kijiji cha Kunzugu, Kata ya Kunzugu wilayani Bunda. Pia wanachama wa shirika wamelima mashamba ya pamba binafsi kuanzia ekari moja na kuendelea.
                                                                                       Shamba la Mfano lililolimwa na shirika la BUFADESO



Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO