Jumapili, 24 Septemba 2017

UZINDUZI MRADI WA KUHAMASISHA JINSIA KUPITIA NYIMBO ZA ASILI TAR 22/9/2017


 BUFADESO inatekeleza mradi wa kuhamasisha jamii kuhusu usawa wa jinsia, ambapo wanachama vikundi walipewa fursa ya Kuandaa Nyimbo zenye ujumbe unao hamasisha usawa wa jinsia na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na mabinti kuanzia ngazi ya familia hadi katika jamii. Ni wazi kuwa jamii yetu ya wilaya ya Bunda inakabiliwa na changamoto ya vitendo vya unyanyasaji wa jinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike. Aidha kutoka na Utamaduni na mila za Makabila mengi ya Mkoa wa Mara, jinsia ya kike imekuwa ikinyanyasika kutokana na matendo kandamizi kama kukeketwa, vipigo kwa wake katika familia, matusi na masimango, watoto wa kike kutopewa kipaumblele cha kupelekwa shule, na kuozwa katika umri mdogo, kunyimwa fursa za umiliki wa rasilimali kama ardhi na mashamba, umiliki wa mali kama nyumba na mifugo mikubwa ikiwemo ng`ombe, wanawake wajane kunyimwa mirathi baada ya waume zao Kufariki na matendo mengine ya kumnyima haki mwanamke kama ushiriki wa masuala mbalimbali ya kijamii. Matendo mengine wanayofanyiwa wanawake yana hatarisha afya zao na muda mwingine hupelekea wanawake kuumizwa, kupewa majeraha au ulemavu na wakati mwingine kusababisha vifo kwa wanawake na kitendo ambacho kinaharibu taifa cha kuwapa watoto wa shule mimba.
Wadau mbalimbali wakifatilia ujumbe uliotolewa katika shughuli ya uhamasishaji wa mradi wa uswa wa jinsia.

Kwa kutambua harakati za serikali katika kushughulikia kumaliza changamoto hii inayokabili jamii zetu ya kutokuwa na usawa wa jinsia na unyanyasaji wa wanawake na wasichana, shirika letu linaunga mkono mapambano hayo na kukemea vitendo vyote vinavyohusiana na kumdhalilisha mwanamke.

Maafisa wa idara za Halmashauri za Wilaya na Mji Bunda kstiks uzinduzi huo

Tunaamini burudani ni njia mojawapo ya kufikishwa ujumbe katika jamii, hivyo kupitia burudani BUFADESO imeona fursa ya Kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya Usawa wa jinsia na kupinga ukatili wa jinsia. Tunaamini kupitia mradi huu unao zinduliwa leo, jamii itapata fursa sio tu kuburudika kupitia burudani zilizo andaliwa bali kupata ujumbe na mwisho wa siku kubadirika na kuacha matendo yanayokiuka utu wa mwanamke. Vikundi wanachama wa BUFADESO vimeandaa Nyimbo na ngoma za kiutamaduni au kikabila zenye ujumbe nzuri unaohamasisha usawa wa jinsia. Nyimbo hizo zinajumuisha Nyimbo za kabila la Wakurya maarufu kama Litungu. Nyimbo za kabila la Waikizu zijulikanazo kama Ndono, Kesa na Bwenga. Nyimbo za Wasukuma Masaligula na Kadumu pamoja na kwaya zenye maudhui ya usawa wa jinsia.
Baada ya Uzinduzi huu, BUFADESO itazunguka katika kata 11 za wilaya ya Bunda tunapofanyia kazi ili kuendeleza kuhamasisha jamii juu ya Usawa wa Jinsia. Pamoja na kuzunguka katika maeneo hayo tofauti, tunaomba ushirikiano wa vyombo vya habari katika kutumia Nyimbo na ngoma hizi zilizo andaliwa ili kuhamasisha jamii juu ya jambo hili. Pia tunaomba serikali iendelee kutia mkazo na kutumia sheria juu ya wananchi wanaoendeleza matendo ya unyanyasaji wa jinsia. Mbali na hayo tuna waasa Wanajamii kutoa taarifa kwenye vyombo husika pale wanapofanyiwa au kuona mwananchi anafanya matendo ya unyanyasaji wa jinsia.

Mwisho kabisa tunaomba na kutoa hamasa kwa jamii hasa watu waliopo vijiji tofauti vya wilaya hii ya Bunda kuacha matendo yote yanayo husiana na kunyanyasa na kukandamiza wanawake na hivyo kusababisha wilaya yetu na mkoa wa Mara kwa ujumla kuwa maarufu kwa sifa mbaya ya Unyanyasaji wa Wanawake. BUFADESO tunaamini kuwa katika familia na jamii yoyote haiwezi kupata maendeleo endapo hakuna ushiriki wa wanawake. Bila ushiriki wa wanawake kuanzia ngazi ya familia shughuli hazitafanyika kwa weledi. Wakulima hawawezi kunufaika na kilimo iwapo mwanamke hapewi fursa ya kushiriki katika shughuli za kutoa maamuzi na mawazo ya kuendeleza kilimo cha familia, hiyo pia haiwezekani katika shughuli za kibiashara, hata katika nyanja ya uongozi; haiwezekani kuwa na ufanisi endapo mwanamke atanyimwa fursa na haki zote anazo stahiki. 

Akizindua mradi huu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili ameilezea jamii kuwa yeye ni mdau mkubwa wa kupinga ukatili wa jinsia. Aidha aliwaasa wananchi kuachana na "mambo ya kale" ya kunyanyasana kwani ni mambo yaliyopitwa na wakati na husababisha kudolola kwa uchumi. Mkuu huyo wa wilaya aliwasisitiza wanacnhi kuachana na mfumo dume na kufanya kazi kwa pamoja. Zaidi aligusia pande zote kuwa wanaonyanyaswa kijinsia sio tu wanawake bali pia wapo wanaume wanaoyanyasika kijinsia na wake zao. Mkuu wa wilaya hii ya Bunda alilipongeza shirika la BUFADESO kwa utekelezaji mzuri wa shughuli zake ikiwemo ya kuhamasisha jamii juu ya usawa wa jinsia.
Mkuu wa wilaya Mwl. Lydia Bupilipili akiongea katika uzinduzi wa mradi wa jinsia, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bunda, Bw. Isaack M. Kabugu na kulia kwake Mwenyekiti wa BUFADESO Edward Chacha
Mwl Lydia aligusa zaidi juu ya shughuli za kilimo kwa wanajamii wa wilaya ya Bunda kwani uchumi wa wilaya hii unategemea zaidi kilimo hasa zao la zao. Mkuu huyu wa wilaya aliwaasa wakulima kurudi kulienzi zao la pamba kwani serikali imeweka mpango mzuri wa kuhakikisha wakulima wanalima kwa tija na kunufaika na kilimo cha zao hilo. aliongezea kuwa serikali imeweka mikakati imara ya zao hilo kuanzia pembejeo hadi mauzo.
Mkuu wa wilaya na viongozi wa BUFADESO wakifurahia burudani na ujumbe kutoka ngoma za kikabila

Jumanne, 12 Septemba 2017

Pakua Nyimbo za Kuhamasisha Usawa wa Jinsia

Shirika la BUFADESO linatekeleza mradi wa kuhamasisha Usawa wa Jinsia na kupinga matendo yanayotokana na mila, tamaduni na mazoea hasi yanayomkandamiza mwanamke na wasichana.
Ili kusikiliza nyimbo hizo unaweza kubonyeza na kufuata maelekezo ya kila wimbo hapo chini:
Litungu - Mutige
Litungu - Tiga Kusara
Kadumu - Ukeketaji
Masaligula - Abhatanzania
Kadumu - Unyanyasaji
Kesa na Bwenga - Mwanaume Sungura
Dogori - Ndoa
Ndono - Haki za Wajane
Neruma Kwaya - Kilio cha Wanawake
Kesa na Bwenga - Tutasala
Masaligula - Wanawake
Boresha Maisha Kwaya - Wanawake wana haki
Dogori - Zinduka

TOZO NA ADA ZILIZOONDOLEWA NA WIZARA YA KILIMO


Chati ifuatayo inaonyesha ada na tozo mbalimbali zilizosamehewa na serikali kupitia Wizara ya Kilimo katika maeneo ya Mazao,  Ushirika, Mifugo na Uvuvi.  Hii ni fursa kwa wakulima, wavuvi na wafugaji kutumia vizuri nafasi ya misamaha hii kuongeza uzalishaji, usindikaji na biashara kwa ujumla. 


Tasnia
Eneo
Idadi ya Ada na Tozo zilizoondolewa
Eneo husika
Mazao
Kahawa
17
Ada kwa ajili ya leseni za: kuuza kahawa ya kijani kwa makampuni na vyama, kuendesha maghala, kuuza premium coffee kwa vyama na makampuni, kukoboa kahawa, kununua kahawa, uendeshaji wa minada

Tozo kwa ajili ya fomu za kuomba:
Kuendesha maghala, kukoboa kahawa, kuuza kahawa (premium), kuuza kahawa ya kijani, kusindika kahawa, kununua kaha
Sukari
16
Ada za kibali cha kuingiza sukari ya viwandani na ile ya kuziba pengo (Sugar Gap), ada ya usajili wa wafanyabiashara wa sukari ya kawaida na viwandani (wakubwa , wadogo na wakati), ada ya kibali cha uingizaji wa sukari ya viwandani nay a kawaida, ada ya leseni mbalimbali kwa uzalishaji wa sukari hapa nchini, ada ya marudio ya leseni mbalimbali kwa wazalishaji wa sukari na ada mbalimbali za leseni ya kuchakata miwa.
Tumbaku
10
Tozo ya Baraza la Tumbaku, ada ya leseni ya kuuza tumbaku nje, leseni ya kununua tumbaku mbichi, Kodi ya leseni ya kununua Tumbaku, Dhamana ya Benk Kuu (1%),  ada ya form ya maombi, Mchango wa ushirika wa mkoa, mchango wa chama cha msingi, gharama za masoko.
Mbegu
7
Tozo kwa ajili ya:- usajili wa muuza mbegu, fomu ya majaribio ya DUS,
fomu ya majaribio ya NPT, Ukaguzi mashambani, Majaribio ya mbegu, kibali cha kusafirisha mbegu, Tangazo la kusafirisha au kuagiza mbegu.
Mbolea
4
Tozo kwa ajili ya Usajili wa mfanyabiashara,
Ada ya leseni, Tozo kwa ajili ya Usajili wa mzalishaji wa mbolea,
Ada kwajili ya Usajili Mbolea
Korosho
2
Ada ya leseni ya kununulia korosho,
Gharama za magunia na Kamba
Pamba
2
Tozo ya kituo cha kununulia pamba, tozo ya maendeleo ya elimu
Chai
1
Gharama za uendeshaji wa vyama vya wakulima (sh 5 kwa kilo)
Mfuko wa Pembejeo
1
Ada ya nyaraka za kuombea mkopo ambayo ni 1% ya mkopo
Ushirika
Ushirika
20
Aina 5 za Ada ya usajili wa mabadiliko ya masharti ya vyama vya  Msingi, Pili, Kati, Shirikisho na vyama vya Ushirika kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja.

Aina 5 za Ada ya uchunguzi  kwenye Rejista ya vyama vya  Msingi, Pili, Kati, Shirikisho na vyama vya Ushirika kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja.

Aina 5 za Ada ya uchunguzi  kwenye Rejista ya vyama vya  Msingi, Pili, Kati, Shirikisho na vyama vya Ushirika kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja.

Aina 5 za Ada ya uchunguzi  wa taarifa za vyama vya  Msingi, Pili, Kati, Shirikisho na vyama vya Ushirika kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja.

Aina 5 za Ada kwa ajili ya utoaji wa nakala za nyaraka   za vyama vya  Msingi, Pili, Kati, Shirikisho na vyama vya Ushirika kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja.  
Mifugo

Maziwa
4
Ada ya usajili wa wadau, Ukusanyaji wa maziwa, usambazaji wa maziwa, Export permit
Nyama
4
Usajili wa wafugaji, usajili wa minada, Export clearance Certificates, Ada ya usajili wa wafanyabiashara wa mifugo na nyama
Huduma za Afya
17
Tozo ya Kibali cha kuingiza ngozi za ng’ombe, Tozo ya Kibali cha kuingiza ngozi za mbuzi/kondoo,  tozo ya kibali cha afya cha kusafirisha Ng’ombe, tozo ya kibali cha afya cha kusafirisha Mbuzi au Kondoo, tozo ya kibali cha afya cha kusafirisha punda au farasi, tozo ya kibali cha kusafirisha ngamia,nguruwe, vifaranga, mayai (Fertilized), mayai ya kula, kuku/kanga, nyama pori, ndege pori, maziwa, mbwa na paka
Uvuvi

Export Royalty
1
Export Royalty
Maendeleo ya uvuvi
4
Movement Permit, ada yaukaguzi wa kiwanda au ghala, Tozo ya cheti cha afya, ada ya usajili wa chombo
Jumla
110


Chanzo ACT

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO