Alhamisi, 13 Oktoba 2022

TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI BUFADESO

 KAMATI YA UCHAGUZI ya shirika la BUFADESO inapenda kuwatangazia wanachama vikundi vya shirika kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la BUFADESO utafanyika kati ya tarehe 13 hadi 16 Disemba 2022. Uchaguzi huo utajumuisha Nafasi zifuatazo:

1)      Mwenyekiti wa Shirika (Nafasi moja)

2)      Katibu wa Shirika (Nafasi moja)

3)      Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi (Nafasi saba)

BUFADESO inawatangazia wajumbe wote wa vikundi wanachama na wanachama binafsi wenye sifa na weledi wa kujaza nafasi hizo kutuma maombi ya kugombea nafasi hizo.

SIFA ZA MWOMBAJI:

1.      Awe mwanakikundi wa kikundi mwanachama hai wa shirika la BUFADESO au mwanachama binafsi wa shirika.

2.      Ajue kusoma na kuandika.

3.      Asiwe muajiriwa wa serikali.

4.      Awe mbunifu mwenye ari ya maendeleo.

5.      Awe mwaminifu na muadilifu.

6.      Awe anayekubali mabadiliko anapopewa changamoto mbalimbali.

 

Mwanakikundi mwenye sifa tajwa na mwenye mwamko wa kuongoza atume barua ya maombi ikiambatana na fomu ya maombi ya kugombea nafasi ya Uongozi iliyojazwa kwa usahihi, inayopatikana kwa watumishi, wawezeshaji jamii, na viongozi wa vikundi:- Fomu hii italipiwa baada ya kutuma maombi kiasi cha Tsh 10,000/- (elfu kumi tu) kupitia akaunti ya shirika benki ya NMB yenye jina la MTANDAO WA WAKULIMA BUNDA namba 30110004259. (Wanawake na vijana wanahamasishwa kugombea nafasi hizo)

 

Maombi yatumwe kwa;

Kamati ya Uchaguzi,

BUFADESO,

S.L.P.95,

BUNDA

 

Mwombaji atume maombi kwa sanduku la posta lililotajwa hapo juu au umpe mwezeshaji jamii au mtumishi wa BUFADESO au afikishe maombi yake katika Ofisi za BUFADESO zilizopo Sazira.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/11/2022 saa kumi na moja jioni.

MUHURI BUFADESO.jpg

Imetolewa na

 

 

KAMATI YA UCHAGUZI

BUFADESO

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO