Shirika
la BUNDA FARMER`S DEVELOPMENT SUPPORT ORGANIZATION (BUFADESO) linalenga
kufanikisha utekelezaji wa miradi na shughuli endelevu. Ili kufanikisha
uendelevu wa shughuli za shirika na miradi ya walengwa yaani jamii, BUFADESO
inatumia WAWEZESHAJI JAMII kufundisha, kuelekeza, Kuunganisha na kuwezesha
wanachama wa shirika na jamii kwa ujumla.
Wawezeshaji Jamii wa BUFADESO wakiwa na Mratibu wa Shirika Ndg. Baraka Kamese
WAWEZESHAJI
JAMII wa shirika la BUFADESO ni wakulima na wafugaji wataalam ambao ni
wanachama wa shirika. Wawezeshaji Jamii hawa wamejengewa uwezo na Shirika la Vi
AGROFORESTRY na kuhitimu mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo mafunzo ya Uimarishaji
wa vikundi, Kilimo na Mabadiriko ya Tabia Nchi, Kilimo Biashara na Ujasiliamali
na Masuala Mtambuka kama Usawa wa kijinsia na Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.
Wawezeshaji
jamii wa shirika la BUFADESO wanafanya kazi kwa kujitolea katika kata na vijiji
wanavyotoka. Kila kata mwanachama wa Shirika la Bufadeso ina wawezeshaji jamii
wawili; mwanaume na mwanamke.
Afisa kutoka Vi AGROFORESTRY Bw. Paschal Paul akitoa somo kwa wawezeshaji jamii wa shirika la BUFADESO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni