Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Mwaka katika eneo la Mkutano Shule ya Sekondari Sazira
Viongozi wa Shirika la BUFADESO
Wasimamizi wa Uchaguzi wakihesabu kura za wagombea nafasi za uongozi wa Shirika.
Msimamizi wa Uchaguzi akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa
Wajumbe wa katika Kikao
Mratibu wa Shirika Ndg. Baraka Kamese akitoa maelezo ya mikakati ya shirika
Mkutano mkuu wa shirika la BUFADESO kwa mwaka huu umefanyika leo siku ya Jumamosi tarehe 14/05/2016 katika Shule ya msingi Sazira. Katika Mkutano Mkuu huu viongozi wapya wa shirika la BUFADESO wataoongoza shirika kwa miaka mitatu ijayo wamechaguliwa. Vingozi waliochaguliwa kuongoza shirika ni Edward Chacha kutoka kata ya Mcharo- MWENYEKITI WA SHIRIKA, Anifa Malegesi kutoka Neruma - MAKAMU MWENYEKITI, Joseph Itoka wa kata ya Wariku - KATIBU MKUU, Juma Salumu kutoka kata ya GuTA - KATIBU MSAIDIZI na Marwa Nyamhanga - MHAZINI WA SHIRIKA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni