Jumatano, 2 Desemba 2015

NJIA ZA KUTENGENEZA NA KUTUMIA MADAWA YA ASILI/KIENYEJI YA KUUA WADUDU WAHARIBIFU SHAMBANI

Utangulizi
            Wadudu  na  magonjwa  limekuwa  tatizo  sugu  na  kero  kwa  wakulima wengi  wa  mazao  nakusababisha  uzalishaji  mdogo  wa  mazao
Ili  mkulima  aweze kupambana  na  tatizo  hili  anaweza  kutumia  mimea  mbalimbali ya  asili  kwakutengeneza  dawa  za asili zikamsaidia  kufukuza  au  kuua   wadudu  waharibifu  wa mazao  shambani.

Madawa  ya  asili  ni  nini
Ni  ujuzi  wote  wa  njia  zinazoelezeka  na zisizoelezeka  za  uchunguzi  zinazohusisha  mimea  ya  asili kutengeneza  madawa ya asili  ya  uzuiaji na uondoaji  wa  hali  isiyo yakawaida  katika  mazao  ya kilimo.

Kwanini  madawa  ya asili
Ni ya asili  kwa  sababu  yametokana  na  mimea  ya  asili.Pia  ni  kitu  kilicho  wazi  na  cha  asili kinachotumika  kufanya  jambo  kwa   kutumia  mimea  ya asili  inayopatikana  katika  maeneo  yetu.
 Kwa hiyo katika  kilimo  ni rahisi  na ni vema  kutumia  madawa  ya  asili  katika  uzalishaji  wa  mazao  ya  chakula ,biashara  na  ufugaji  ili  yaweze  kukusaidia  katika mambo  yafuatayo:-
Ø  Kusaidia  katika  matumizi  bora  ya ardhi.
Ø  Kusaidia  katika  kuzalisha  chakula  bora  na  salama.
Ø  Kusaidia katika  kulinda  Afya  ya  mkulima  na  jamii  kwa  ujumla.
Ø  Kusaidia katika kuzalisha  bidhaa  bora  zitokanazo na mazao na  hatimaye  kujipatia  kipato(soko- ndani  na nje  ya  nchi).
Ø  Kusaidia  mkulima  kujiwekea  akiba  ya  fedha.
Ø  Kusaidia  uboreshaji  wa  mazingira  wa  muda  mrefu.
Ø  Kusaidia  kukomesha/kupunguza  wadudu  na  magonjwa  kwenye  mashamba  ya  wakulima.
Ø  Viuatilifu  asilia  vinaweza  kuoteshwa  nyumbani  au  kwenye  eneo  lako  la  shamba  na  kupunguza  gharama  za ununuzi  wa madawa.
Ø  Kuthibiti  wadudu  na magonjwa  kwa  njia  ya  asili  kunalenga  kupunguza  milipuko  ya  magonjwa  kupitia  kilimo  endelevu  ambapo    mifumo  ya kilimo  inaendana  na  mazingira  ya  asili.
Ø  Hata  hivyo  ukikumbana  na  wadudu  waharibifu  popote  pale  shambani  kwako  ni  rahisi   sana  kuandaa  na  kutumia  viuatilifu  asilia  wewe  mwenyewe  kuwathibiti  kuliko  unavyofikiria.
Baadhi  ya mimea  itumikayo  kufukuza /kuua  wadudu  waharibifu  ni  kama  ifuatayo:-
VITUNGUU  MAJI(Allium  cepa)Onion
               Mmea  huu  husaidia kufukuza  wadudu  na  kuondoa  fangasi  kwenye  mimea  ya mbogamboga
   na matunda.Huondoa  aphids  ambao  hushambulia  Kabichi,inzi  nyanya  ,funza  vitumba(fruit  worm),inzi  weupe(white  flies),minyoo  fundo(root knot nematodes)na  utitiri(redspidermites).

Magonjwa:
Bakajani(early  and  late  blight)

Sehemu  za  kitunguu maji  zinazotumika ni  kitunguu  chenyewe  au majani yake.

Jinsi  ya kutumia
§  Menya  kitunguu  pondaponda  au  chukua   majani  yake  kiasi  cha  gram  100 pondaponda
§  Changanya  na  maji  lita  moja
§  Funika  na acha  vitulie muda  wa siku  saba.
§  Baada  ya  siku  hizo  kamua  ondoa  makapi ,tumia  mara  moja  kwa  mimea  iliyo  athirika.
Wakati  mwingine  mimea hupandwa  kwa  kuchanganya na vitunguu maji  ili  kufukuza  wadudu  wanaoshambulia  mimea hiyo.mf mistari  ya miche  ya  kabichi  huchanganywa  na mistari  ya miche  ya vitunguu maji au mistari  ya  karoti  na mistari  ya vitunguu  maji.

Matumizi  mengine
·         Ni  kiungo  cha  chakula(food  flavouring)
·         Huponya  magonjwa(antibiotics)
·         Huponya  vidonda(antiseptic)

NB Andaa  dawa  kulingana  na  ukubwa  wa  shamba.
Ikumbukwe  kuwa  tutumiapo  dawa  yoyote  yakunyunyizia  kwenye  mazao  shambani  hasa  mboga  na matunda  tusivune  mboga hizo  au  matunda  kabla  ya wiki moja- wiki mbili(2)

ONYO
              Majimaji  ya  kitunguu  huwasha macho  menya  kwa uangalifu.
VITUNGUU  SWAUMU(Allium  sativum)
Hufukuza  wadudu,huondoa  fangasi, minyoo  fundo(nematodes)

Jinsi  ya  kutengeneza
Viwango  tofauti  hutumika kufuatana  na ugumu wa wadudu
Ø  Twanga  vitunguu  swaumu  1-3
Ø  Changanya  na  lita  moja  ya  maji
Ø  Changanya  na  sabuni  kidogo
Ø  Tumia  mara moja  kwenye  mimea  iliyo athirika.

-Kitunguu  swaumu  kinaweza  kutwangwa,kukaushwa  na kusagwa kikawa  unga  na  kikatumika  kama  dawa  unga  kwenye  nyanya  zilizougua  baka  jani(blight).
-Vitunguu  swaumu  vikipandwa  kuzunguka  mimea  ya  matunda  na mbogamboga nyingine  hufukuza  minyoo  fundo(aphids),mchwa,panya  na wadudu  wanaotoboatoboa  shina  la mche.

ONYO
Vitunguu  swaumu  ni  dawa  ambayo  inaweza  kuua  viumbe  hata  wenye  manufaa ardhini  na  wale  waharibifu  .Tumia  dawa   kwenye  mimea  yenye  umri  wa mwezi  mmoja  nakuendelea.Pia  usitumie  daw a hii kwenye  mimea  jamii  ya  mikunde(leguminous  plant).
     
   PILIPILI KALI/PILIPILI KICHAA(chill)
Pilipili  ni  dawa  inayofukuza  wadudu  wote  shambani  wanaotambaa  na wanaoruka.

Pia  pilipili  huondoa  fangasi  kwenye mimea  bacteria  na  virusi.



Maoni 1 :

  1. Dawa ya kuua utitiri kwenye mbwa, paka na kuku ni ipi.Iwe ya asili maana za viwandani hazifanyi kazi pamoja na ughali wake.

    JibuFuta

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO