Mwaka 2009 Vi AGROFORESTRY ilibadirisha mfumo wa utendaji toka ngazi za vijiji kwenda ngazi ya kata.
Mbinu zilizotumiwa ni pamoja na
- Kutembelea mkulima mmoja mmoja
- Kutoa mafunzo mbalimbali kupitia vikundi vya wakulima.
- Kutoa elimu kupitia taasisi hasa mashule
- kufanya kampeni za uhamasishaji hasa utunzaji wa mazingira
- mikutano na hadhara
- mashamba darasa.
Shughuli zikitekelezwa na shirika la VI AGROFORESTRY ni pamoja na:-
- Ujengaji uwezo kwa kuhamasisha uanzishaji, uimarishaji na uendeshwaji wa vikundi ambapo vikundi 437 vilianzishwa.
- uhamasishaji juu ya matumizi ya mfumo wa kilimo mseto kwa wakulima.
- Elimu ya mabadiriko ya tabia nchi.
- ujasiriamali
- ushawishi na utetezi
- masuala mtambuka: masuala ya usawa wa kijinsia, UKIMWI na virusi vya Ukimwi
Tarehe 7 Disemba 2015, Shirika la Vi Agroforestry lilifanya mkutano na wadau ikiwemo serikali na kutangazakuwa kuanzia mwaka 2016, shughuli zilizokuwa zinafanywa na shirika la Vi zitakabidhiwa kwa shirika la Wakulima lililoanzishwa na vikundi vya wakulima, wafugaji na wavuvi wilayani Bunda, BUFADESO. Katika mkutano huo, shirika la Vi AGROFORESTRY lilitoa vyeti kwa wawezeshaji jamii wa BUFADESO waliopatiwa na kufuzu mafunzo mbalimbali.
Meneja wa Vi na Mkuu wa kitengo cha Ujengaji wa Ubia katika mkutano
Mtaalamu wa Vi akisoma ripoti ya utekelezaji wa shughuli
Baadhi ya washiriki katika mkutano
Mwenyekiti wa BUFADESO akitoa maelezo
Muwezeshaji Jamii akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo kutoka Vi AGROFORESTRY
Muwezeshaji Jamii akipokea cheti
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni