Kila shirika
la kiukulima tunalikumbusha kusimamia misingi mikuu ya shirika ili kuweza kutoa
huduma nzuri na zenye tija kwa wanachama wake.Miongoni mwa misingi hiyo ni
pamoja na
- Shirika lisijihusishe na siasa au
dini.
- Shirika lisiwe na ubaguzi /
ubinafsi katika vikundi vilivyopo katika kata na vijiji.
- Shirika liwe linafanya shughuli zake katika kata
husika na vijiji husika kwa mujibu wa usajili.
- Shirika liwe linashughulika na vikundi vya wakulima na wafugaji na
siyo vinginevyo.
- Shirika liwe na shughuli zinazo
onekana na kupimika na zisiwe za kutegesha
- Shirika liwe na uongozi imara
unaofata misingi ya utawala wa kanuni na sheria za shirika na nchi, usio
na harufu ya rushwa.
- Shirika liwe na miongozo
inayotafsiri zana ya usimamizi na mifumo ya shirika
- Shirike lijikite kusimamia DIRA, DHAMIRA na MALENGO YAKE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni