NINI
MAANA YA MPANGO:
·
Ni mlolongo wa mawazo, shughuli, michakato au
matendo; ulioandaliwa kwa wakati uliopo ili uweze kutekelezwa au kufanyiwa kazi
wakati ujao.
·
Kwa kifupi ni matarajio na matazamio ya
mambo/shughuli za kufanya baadae.
·
Shirika linaweza kuwa na mipango tofauti kama
vile mpango kazi, mipango ya bajeti, mipango ya uongozi na utawala, mpango
mkakati n.k
Kupanga ni nini?
1.
Kupanga
ni kuchagua.
2.
Kupanga
ni kuchukua picha ya yaliopita, kulinganisha na hali ya sasa ili kuleta matokeo
bora.
3.
Kupanga
ni mchakato wa kueleza na kuelewana miongoni mwa watu wanaofanya kazi pamoja
ili kuleta mabadiliko fulani.
4.
Kuweka
msingi wa maamuzi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za miradi.
KWA
NINI TUNAHITAJI KUPANGA?
Ø Ili kupanga
rasilimali za mradi na kufikia matokeo bora iwezakanavyo ili kufikia malengo.
Ø Kujua rasilimali
zinazotakiwa, muda, uhalisia n.k.
Ø Kuweka malengo
kwa shughuli za mradi.
Ø Kuamua viashiria
vya ufuatiliaji na tathimini na muundo wa utoaji taarifa.
Ø Kuratibu na
kushirikiana na wengine ili kuepuka upotevu wa muda, vifaa, fedha, nguvu,
nishati n.k.
Ø Kuhakikisha
mfuatano bora wa utekelezaji wa shughuli ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima.
Ø Kupata mwongozo
wa bajeti.
Ø Kufanya
maandalizi kabla ya utekelezaji ili kufahamu shughuli tunazowajibika
kuzitekeleza.
v Kwa kuwa mambo
haya yanalenga kupata matokeo bora, bila shaka kunahitajika zana bora.
v Kwa mtu yeyote
anayetarajia kufanya shughuli yoyote, lazima ahakikishe kuwa nyenzo zake za
kazi ni bora. Mfano Mkulima anahitaji jembe bora.
Mchoraji anahitaji brush
bora.
v Zana ya shirka
katika kupanga ni DIRA.
MAANA
YA MKAKATI:
n Mkakati kwa
maneno rahisi ni mpangilio katika mtiririko wa maamuzi. Hujumuisha mambo yanayolenga kufikia hali endelevu katika
ushindani. Mkakati unahusiana na shauku ya kuwa tofauti kwa kuleta matokeo
chanya.
MAANA
YA MPANGO MKAKATI
·
Ni mchakato maalumu unaolenga kutambua na kufanyia
kazi mambo/shughuli/changamoto anuai kwa njia shirikishi ili kufikia matokeo
yanayolengwa.
·
Mpango Mkakati ni mpango wa jumla wa maendeleo
ya taasisi husika unaopangwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
ü Changamoto
zinazoikabili taasisi husika katika mazingira ya ushindani
ü Hali
halisi ya mazingira ambamo taasisi hiyo imo
ü Uwezo
wa taasisi husika katika kutekeleza majukumu yake
ü Dira,
dhamira na malengo ambayo taasisi imejiwekea
ü Sera
na sheria za nchi zinazotawala shughuli za taasisi husika
·
Mpango mkakati unahusisha mchakato wa
kuchanganua hali ya ushindani wa taasisi, kutayarisha dira, dhamira na malengo
ya taasisi, kuandaa mpango wa utekelezaji na kutafuta rasilimali zitakazosaidia
kufikia malengo yaliyowekwa.
·
Ili mpango uwe mpango mkakati ni LAZIMA:
-Uonyeshe
muelekeo wa wapi tunalenga kufika.
-Uwe
na muda maalumu wa kufikia matarajio.
-Kuwe
na malengo ya muda mfupi na muda mrefu.
-Kuwe
na vipaumbele vya miaka mf miaka 3, 5 au 10
FAIDA ZA KUWA NA MPANGO MKAKATI KATIKA SHIRIKA
i. Unapunguza uwepo wa ushindani na kurahisisha
fursa ubia na mashirika/taasisi nyingine.
ii.
Unatoa picha ya wazi ya nini shirika linafanya.
iii.
Unasaidia kutambua na kufikia dira, dhamira na malengo ya shirika.
iv.
Unaleta dhana ya Umiliki.
v.
Unachochea uwajibikaji kwa matokeo mazuri.
vi.
Unahamasisha wafadhili na mashirika mengine kusaidia shirika.
vii.
Unaainisha uwazi wa utendaji kazi kwa washiriki.
viii.
Unarahisisha tathmini ya muda na shughuli.
ix.
Unaainisha walengwa wa shughuli.
x.Huunda
mazingira ya kufanya maamuzi.
KWA NINI SHIRIKA
LINAHITAJI MPANGO MKAKATI?
(a)
Mpango mkakati Unasaidia shirika kuwa na
utawala/uongozi bora.
(b)
Unawezesha shirika kuweza kutofautishwa na
mashirika/taasisi nyingine zinazofanya kazi zenye kufanana na shirika letu.
(c)
Unasaidia shirika/taasisi kutengeneza sera.
(d)
Mpango mkakati unasaidia shirika/taasisi
kuaminika na kupewa mtazamo mzuri
(e)
Unasaidia shirika kuwa na umakini na uwazi
katika utendaji wa shughuli zake.
(f)
Unasaidia
shirika kuwajibikia/kufanya maamuzi kabla ya matokeo na si baada ya
matokeo
(proactive rather than reactive)
NI MUDA GANI SHIRIKA LINATAKIWA KUANDAA MPANGO MKAKATI
1)
Pale shirika linapoanzishwa.
2)
Pale dira, dhamira na vipaumbele vya shirika
vitakapobadirishwa.
3)
Pale sababu za nje zinapoathiri na kuleta
mgongano katika shirika.
4)
Pale shirika linapohitaji kuongeza malengo yake.
TAARIFA/NYARAKA ZINAZOHITAJIKA WAKATI WA KUANDAA MPANGO MKAKATI:
I.
Katiba ya shirika.
II.
Muundo wa shirika.
III.
Ripoti za shirika.
IV.
Sera za serikali
V.
Mpango mkakati wa nyuma
VI.
Ripoti za tathmini ya mahitaji
VII.
Upembuzi yakinifu/utafiti wa majaribio
VIII.
Malengo na shughuli za shirika.
IX.
Mpango mkakati wa shirika mama au shirika rika.
MCHAKATO WA KUTAYARISHA MPANGO MKAKATI
·
Mchakato wa kutayarisha mpango mkakati kwa
kawaida hufuata hatua kuu nne muhimu kama ifuatavyo:
(a) Uchambuzi
wa hali halisi
·
Ni ipi hali halisi ya taasisi kwa sasa?
·
Hatua hii inahusisha uchambuzi wa taasisi
yenyewe na mazingira yanayoizunguka
·
Lengo la kuichambua taasisi husika ni kufahamu uwezo (strengths) na udhaifu (weaknesses) wake. Uchambuzi
huu hufanywa kwa kuangalia dira, dhamira na malengo ya taasisi husika.
·
Lengo la kutathmini mazingira yanayoizunguka
taasisi ni kutaka kupata ufahamu wa fursa
(opportunities) na vikwazo (threats)
vya taasisi husika.
Kazi
ya wana Bodi: Chambua hali halisi ya shirika letu la BUFADESO
(b) Uandaaji wa mpango mkakati
·
Taasisi inataka kuwa ya namna gani?
·
Kutayarisha dira, dhamira na malengo ya taasisi
·
Kuandaa mpango wa maendeleo ambao unaonyesha
malengo, matendo/shughuli, muda wa utekelezaji, wahusika, rasilimali na
viashiria vya ufanisi
Kazi: Fafanua dira na dhamira ya shirika letu
(c) Utekelezaji wa mpango
·
Taasisi itafikaje kule inakotaka kufika?
·
Wakati wa utekelezaji wa mpango sharti taasisi
izingatie muundo wake wa utendaji, kugawa rasilimali kwa kufuata vipaumbele,
kuhakikisha kuwa watumishi waliopo wanatosha na wana ujuzi unaotakiwa.
·
Mpango wa utekelezaji wa mwaka pamoja na bajeti
huandaliwa kwa kuzingatia uwezo wa taasisi husika
·
Baada ya fedha za utekelezaji kupatikana mpango
kazi huandaliwa ukiwa ni mwongozo wa utekelezaji
Kazi: Chora muundo wa shirika letu
(d) Ufuatiliaji na tathmini ya mpango
·
Taasisi itajuaje kwamba imefika mahali
ilipokusudia?
·
Ufuatiliaji hufanywa ili kufahamu ni kwa kiasi
gani taasisi imefikia malengo yake kwa kuzingatia dira na dhamira.
·
Kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini taasisi
huweza kuchukua hatua za marekebisho pale ambapo mambo hayajaenda vizuri. Iwapo
mpango kazi hautekelezeki vizuri, Yapaswa malengo, shughuli au mikakati
inayotumika haijawekwa vizuri, au haitekelezeki na hivyo marekebisho yaweza
kufanywa kwenye lengo au mikakati inayotumika.
Swali:
Ni zana ipi inatumika katika ufuatiliaji na tathmini katika shirika lenu
MUUNDO WA MPANGO MKAKATI
1.
UTANGULIZI:
Katika kipengele hiki, unaweza
kuwatambua au kuwashukuru wadau waliowezesha Shirika kwa namna moja au
nyingine.
2. UTAMBULISHO:
Kutambulisha shirika kwa ufupi
kuhusu aina ya Shirika, jinsi lilivyoanzishwa na kusajiliwa, eneo la kazi na Idadi ya wanachama.
3. DIRA,
DHAMIRA, MAADILI NA WALENGWA
DIRA
Dira ya Shirika
ni ndoto/maono/taswira ya kifikra ya jinsi mafanikio ya mbele yatakavyo kuwa.
Dira huelezea ni vipi/nini shirika linahitaji kuona miaka ya mbele. Dira huweka
msingi imara katika shughuli mkakati. Huwezesha kufanya uchanganuzi wa mipango
mkakati na shughuli. Kwa hali hiyo dira ni sehemu muhimu katika mchakato wa
kupanga kimkakati
UBORA
WA DIRA
Ukitaka
kuhakikisha ubora wa
dira yako, jiulize
maswali yafatayo:
1: Je, inaelekeza kile ninataka kufikia?
2: Je, inaendana
na shughuli ninazo
kusudia kufanya?
3: Iko wazi kiasi
cha kuvunjwa katika malengo
kadhaa?
4: Ipo wazi kiasi
cha kuelewaka kwa watu, kushawishi
na kusisimua?
5: Inaweza
kuandaa juhudi mioyoni mwa
watu na
kujitoa?
DHAMIRA
Dhamira ni
wito/utume wa shirika unaojumuisha shirika litafanya vipi {kazi ya muda mrefu}
kufikia dira.
Dhamira hueleza
shughuli na kiwango
cha shughuli zinazotekelezwa na
shirika au taasisi
DHAMIRA YAWEZA
KUFANYA NINI?
Dhamira inaeleza shughuli za shirika inajibu swali:
Kwa nini tuko hapa?
Huelezea kiwango. Nani tunamhudumia na kwa namna gani?
Huonesha
mwelekeo na mkakati
mkubwa unaokua kiongozi
kwa maamuzi ya
ngazi ya chini
Hujibu , tunashirikije
sisi kama wanachama
wa shirika ili
kuleta mapinduzi?
KUELEWA KAMA
DHAMIRA NI SAHIHI
Tujiulize maswali
yafuatayo
-
Inaeleweka?
-
Inafikika?
au ni ya kufikirika?
-
Inaelezea mambo ambayo shirika linayalenga?
- Shirika
linamhudumia nani?
- Inaendana
na
ü
Dira yangu
binafsi?
ü
Dira ya wadau?
ü
Dira ya shirika?
MAADILI;
Haya ni matamko yanayobainisha falsafa
shirikishi za shirika
Matamko haya yana
kazi gani ?
·
Hutoa
misingi ,kanuni na
imani zinazolinda menejimenti
ya shirika mahusiano
ya wafanyakazi na
mahusiano ya wadau
na shirika
·
Hueleza
viwango muhimu na
tabia zinazotakiwa na shirika
·
Hueleza
tunavyohusiana na kuwasiliana
sisi kwa sisi
na wadau pia
·
Hufafanua
namna tunavyofikia maamuzi
·
Huelezea
tunavyotumia muda wetu .
KUTAMBUA USAHIHI
WA MAADILI HUSIKA
Ujiulize
-
Yana hasisha
?
-
Yameshilikishwa
/ Kila mtu
anayafahamu ?
-
Yanaonyesha
vipaumbele ?
-
Yanaonesha
miongozo ?
-
Yanaainisha
tabia zisizotakiwa ?
-
Yanaendana
na dira na
dhamira za shirika?
WALENGWA
Walengwa wa Shirika, hawa ni wahusika wanaotarajiwa kunufaika na kutokana na shughuli
ambazo shirika linafanya.
4. MUUNDO
WA SHIRIKA:
Muundo wa shirika ukoje kuanzia
ngazi ya juu ambayo ni uongozi mpaka ngazi ya chini yaani walengwa. Muundo
uonyeshwe katika mchoro.
5. UCHAMBUZI
WA HALI/MAZINGIRA:
Uchambuzi wa Mazingira ya ndani:
Hali halisi ya shirika ikoje kwa sasa. Hapa uwezo na udhaifu wa Shirika
utaainishwa.
Pia uchambuzi wa mazingira ya nje
ni vizuri uainishwe ili kubainisha fursa zinazoweza kusaidia shirika katika
kufikia malengo yake, au vikwazo vinavyoweza kukwamisha shughuli za shirika.
Uchambuzi utaangalia nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiteknolojia.
6.
MALENGO, SHUGHULI NA MATOKEO TARAJIWA:
MALENGO
Malengo ni hatua ambayo shirika
halijafikia na hivyo linataka kufikia hatua hiyo. Yapaswa kufafanua lengo
husika ambalo linataka kufikiwa. Malengo yanawekwa kwa kuzingatia vipaumbele
vya shirika.
Hapa tunapata
lengo kuu na
malengo madogomadogo
Huainisha mambo
dhahiri yatakayofikiwa .
Malengo huangalia
nje zaidi (Siyo
tunataka kuwa)
-
Huonesha
yatavyopimwa
-
Hujibu
dhamira
- Kuonesha
mambo
yatakayo sisitizwa
Malengo hutoa
mwongozo wa vipi tutajipanga au
tutakavyotenda kufikia matokeo
KUTHIBITISHA USAHIHI
WA MALENGO
Ili kujua kama malengo ya shirika letu ni sahihi tujiulize
maswali yafuatayo:
- Yanaweza kuonekana
?
- Yanapimika ?
- Ni dhahili ?
- Tumeyawekea vipaumbele ?
- Yanaendana na dira
na dhamira ya shirika letu?
SHUGHULI
Shughuli ni kazi
ambazo shirika litazifanya kwa wakati husika kulingana na malengo ili kuleta
matokeo tarajiwa.
MATOKEO TARAJIWA;
Ni vitu vitakavyotoa ushahidi wa mafanikio au hasira ya
shughuli au mradi uliofanyika. Yanaweza kupimika kwa Idadi (yanaweza
kuhesabika) au kupimika kwa kiwango cha ubora.
Kwa nini matokeo
tarajiwa ni muhimu ?
n
Ni kama nyenzo
ya kuangalia mwenendo wa shughuli za shirika na pia husaidia kutambua
kama matatizo.
n
Husaidia kutambua hali itakavyokuwa siku za
mbeleni.
n
Yanapolinganishwa na malengo, matokeo tarajiwa
huweza kuonyesha kama hatua za kinidhamu
zitahitajika kuchukuliwa na uongozi ili kurekebisha tatizo lililojitokeza,
huweza kutathimini umakini wa watendaji kstika uchukuaji hatua na pia hutoa
ushahidi wa namna gani malengo yamefanikiwa.
7. MIKAKATI
Mikakati ni mbinu/njia zitakazotumika katika kutekeleza shughuli za
Shirika ili kufikia malengo. Yapaswa kuelezea na kufafanua ni mikakati ipi
itatumika wakati wa kutekeleza
8.
MPANGO KAZI;
Huonyesha ni
jinsi gani utekelezaji wa miradi utakavyokuwa kwa vipindi na kwa ujumla, pia
huelezea rasilimali gani zitahitajika katika utekelezaji wa mradi/miradi
iliyoainishwa na pia huonyesha makisio ya bajeti yatakavyo kuwa kulingana na
mahitaji ya utekelezaji wa miradi
husika.
Katika mpango
kazi tunajiuliza
1. Nani
atafanya nini?
2. Nini
kitafanyika lini? Na kitafanyikanye?
3. Nini
kitafanywa wapi?
4. Vitu
gani vinahitajika?
5. Gharama
zake ni kiasi gani?
6. Matarajio
ya kufanya nini ni yapi?
LENGO
|
SHUGHULI
ZITAKAZOFANYIKA
|
MUDA
|
RASILIMALI
|
GHARAMA
|
WALENGWA
|
MFUATILIAJI
|
MATOKEO
TARAJIWA
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Chati namba 1:
MPANGO KAZI
MATUMIZI
|
Mwaka 1
|
Mwaka 2
|
Mwaka 3
|
Mwaka 4
|
Mwaka 5
|
JUMLA
|
Shughuli za miradi
|
|
|
|
|
|
|
Uendeshaji wa shirika
|
|
|
|
|
|
|
JUMLA KUU
|
|
|
|
|
|
|
Chati namba 2:
MAKISIO YA BAJETI
9. UFUATILIAJI
NA TATHIMINI
Kipengele hiki huelezea kwa ufupi mipango ya asasi katika kusimamia na kutathimini mwenendo wa kazi ili kuweza kupima mafanikio kwa kutoa ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo:-
Kipengele hiki huelezea kwa ufupi mipango ya asasi katika kusimamia na kutathimini mwenendo wa kazi ili kuweza kupima mafanikio kwa kutoa ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo:-
i.
Mbinu gani zitatumka
ii.
Dhana zitakazotumka
iii.
Kila baada ya muda gani
iv.
Nani watakaohusika na zoezi hilo n.k
KUMBUKA:
Malengo
ni ufunguo wa mafanikio & Kupanga ni
kuchagua
Yoh 3:16 Kuikomboa
sayari hii ulifanyika mpango
Josh 6: 1-7 Mji
wa Yeriko ulitekwa kwa mpango
Na,
Baraka Kamese