TAARIFA KWA UMMA
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anatarajia kuhakiki Mashirika yote
Yasiyo ya Kiserikali kuanzia tarehe 21 hadi 31 Agosti, 2017. Lengo kuu la
zoezi hili ni Kuhuisha orodha ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini,
Kuboresha Kanzi Data ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kupima utekelezaji
wa majukumu ya Mashirika haya. Zoezi hili litafanyika katika Kanda tano (5).
Kanda ya Mashariki itahudumia mikoa ya DAR ES SALAAM, LINDI,
MTWARA, PWANI na MOROGORO na Kituo kitakuwa Idara ya Uratibu wa
NGOs DAR ES SALAAM; Kanda ya Kati itahudumia mikoa ya DODOMA,
SINGIDA, TABORA na KIGOMA na Kituo kitakuwa DODOMA, Makao Makuu
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyopo
Chuo Kikuu cha Dodoma, Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya
Jamii, Jengo Na. 11, Dodoma; Kanda ya Kaskazini itahudumia mikoa ya
KILIMANJARO, TANGA, ARUSHA na MANYARA na Kituo kitakuwa katika
Ofisi ya Katibu Tawala (M) KILIMANJARO; Kanda ya Ziwa itahudumia mikoa
ya MWANZA, KAGERA, MARA, GEITA, SIMIYU na SHINYANGA na Kituo
kitakuwa katika Ofisi ya Katibu Tawala (M) MWANZA na Kanda ya Nyanda za
Juu - Kusini itahudumia mikoa ya MBEYA, RUVUMA, KATAVI, RUKWA,
SONGWE, NJOMBE na IRINGA na Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu
Tawala (M), MBEYA.
Wakati wa uhakiki kila shirika linapaswa kuwasilisha Cheti Halisi cha Usajili,
Nakala ya Cheti cha Usajili, kujaza fomu ya uhakiki NGO-Fomu/UHK/2017
inayopatikana katika Tovuti (www.tnnc.go.tz), Stakabadhi za Malipo ya Ada ya
mwaka toka kuanzishwa kwa shirika, Barua kutoka kwa Afisa Maendeleo ya
Jamii (Mkoa/Wilaya/Halmashauri/Manispaa) ikithibitisha uwepo wa Ofisi ya
Shirika na nakala ya katiba iliyothibitishwa na Msajili wa NGOs. Aidha,
Mashirika yote yatakayoshindwa kuhakikiwa katika vituo vya Kanda tajwa
hapo juu, yatafutiwa Usajili na kuondolewa kwenye Regista ya Msajili wa
NGOs. Ili kutoa fursa ya kuhuisha Kanzi Data na Benki ya Takwimu, Usajili wa
NGOs utasitishwa kuanzia tarehe 21 Agosti hadi 30 Novemba, 2017.
M.S. Katemba
MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Kauli mbiu yetu
BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima
MUHIMU
Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni