Ijumaa, 1 Februari 2019
TAARIFA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Kaimu Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anapenda kuyakumbusha
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuwasilisha Taarifa za mwaka 2018
kwa mujibu wa kifungu Na. 29 (a) & (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 na Kanuni Na. 10 ya Kanuni za Sheria ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 (GN 152, 2004) kama
ilivyorekebishwa na Kanuni Na. 6 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali ya mwaka 2014 (GN 8, 2015), kabla ya tarehe 15 Aprili, 2019.
Taarifa hiyo ijumuishe Taarifa za utendaji kazi, Taarifa za fedha
zilizokaguliwa, NGO Fomu Na. 10 na malipo ya ada ya mwaka. Mashirika
yatakayoshindwa kutekeleza agizo hili ndani ya kipindi husika,
yatachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
Kauli mbiu yetu
BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima
MUHIMU
Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO