Ijumaa, 2 Desemba 2022

Welcome to our online launch and panel discussion

 


Are you a development practitioner, policymaker or researcher engaging in sustainable agriculture, biodiversity, rural livelihoods or perhaps food security? Would you like to learn about how agroforestry as a method could be scaled up? Welcome to the launch of a new policy brief by Agroforestry Network.

Date: Monday 12 December 2022

 

Time: 14.00-15.00 CET

 

Place: Online on Teams. Register here

 

Panel:

  • Elaine Springgay, Food and Agriculture Organisation of the UN, FAO
  • Judit Csikvári, European Agroforestry Federation, EURAF
  • Elisabeth Simelton, Swedish International Development Cooperation Agency, Sida
  • Emilie Molin, Swedish Ministry of Enterprise and Innovation
  • Sara Furenhed, Swedish Board of Agriculture
  • Linnéa Pasquier, main author of the policy brief, Agroforestry Sweden

Moderator: Charlotta Szczepanowski, Vi Agroforestry (Vi-skogen)

 

The policy brief in short:

Agroforestry can provide solutions for increasingly urgent challenges posed by climate change, biodiversity loss, food insecurity, and other global issues, as well as improve ecosystem services, local economies and rural livelihoods. The brief focuses on opportunities, barriers and actions for spreading agroforestry systems more widely. In addition, the brief provides recommended actions to support the upscaling of agroforestry.

 

The policy brief Scaling up agroforestry will be made available on agroforestrynetwork.org on December 12th.

 

Organizer: 

Agroforestry Network – a platform for international agroforestry practise, based in Sweden.

 

Contact:
For questions about the event, please contact Åsa Ljusenius 
asa.ljusenius@viskogen.se

Ijumaa, 4 Novemba 2022

TANZANIA YAHAKIKISHIWA SOKO LA UHAKIKA LA PARACHICHI NCHINI MAREKANI

Kufuatia mahusiano mazuri ya kibiashara baina ya Tanzania na Marekani,Tanzania ipo mbioni kunufaika na soko kubwa la Parachichi nchini Marekani baada ya kukamilika kwa taratibu chache za masuala ya usafi wa mazao.


Hayo yamesemwa leo tarehe 03 Novemba, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Kilimo  Mh.Anthony Mavunde na Ujumbe kutoka nchini Marekani ukiongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Jewel Bronaugh

"Serikali inaendelea na mazungumzo na Marekani, ili tuweze kufikia vigezo vya kibiashara kuuza parachichi yetu nchini mwao. Tayari taratibu za awali za kuhakikisha tunakidhi vigezo vya kimataifa vya usalama na usafi wa mazao umeanza,kukamilika kwa taratibu hizo kutafungua mlango wa nchi ya Tanzania kuanza kusafirisha kwa wingi parachichi nchini Marekani na hivyo kutengeneza soko la uhakika la zao la parachichi kwa wakulima wa Tanzania.


Ninaishukuru Serikali ya Marekani kwa kukubali kuirudisha Tanzania kuwa moja ya Nchi zinazotekeleza Programu ya  Feed the Future ambao pia ndani yake upo mradi wenye thamani ya Dola za kimarekani 40milioni wa kukuza tasnia ya mbogamboga na matunda ambao pia utalenga katika kuongeza mnyororo wa thamani ya zao la parachichi na mazao mengine.


Ni vyema programu mbalimbali zinazoletwa kutekelezwa nchini ziwe zinaendana na mipango ya Serikali ambayo inalenga kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wakulima na Watanzania kwa ujumla ili kupunguza fedha nyingi kutumika katika semina na warsha mbalimbali ambazo mwisho wa siku zina mchango mdogo katika kukuza sekta ya Kilimo”Alisema Mavunde


Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Kilimo wa Marekani, Dkt. Jewel Bronaugh ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira na utashi mkubwa wa kukuza sekta ya kilimo ambayo inathibitishwa na ongezeko la bajeti ya nchi katika kilimo na kuja na mikakati kabambe ya kukuza sekta ya Kilimo nchini.


Naibu Waziri Dr.Bronaugh ameahidi nchi yake kuendelea kuipa ushirikiano Tanzania kwa kuendelea kutekeleza programu na mikakati mbalimbali yenye lengo la kuendeleza sekta ya kilimo na kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya Marekani na Tanzania.

Alhamisi, 13 Oktoba 2022

TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI BUFADESO

 KAMATI YA UCHAGUZI ya shirika la BUFADESO inapenda kuwatangazia wanachama vikundi vya shirika kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la BUFADESO utafanyika kati ya tarehe 13 hadi 16 Disemba 2022. Uchaguzi huo utajumuisha Nafasi zifuatazo:

1)      Mwenyekiti wa Shirika (Nafasi moja)

2)      Katibu wa Shirika (Nafasi moja)

3)      Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi (Nafasi saba)

BUFADESO inawatangazia wajumbe wote wa vikundi wanachama na wanachama binafsi wenye sifa na weledi wa kujaza nafasi hizo kutuma maombi ya kugombea nafasi hizo.

SIFA ZA MWOMBAJI:

1.      Awe mwanakikundi wa kikundi mwanachama hai wa shirika la BUFADESO au mwanachama binafsi wa shirika.

2.      Ajue kusoma na kuandika.

3.      Asiwe muajiriwa wa serikali.

4.      Awe mbunifu mwenye ari ya maendeleo.

5.      Awe mwaminifu na muadilifu.

6.      Awe anayekubali mabadiliko anapopewa changamoto mbalimbali.

 

Mwanakikundi mwenye sifa tajwa na mwenye mwamko wa kuongoza atume barua ya maombi ikiambatana na fomu ya maombi ya kugombea nafasi ya Uongozi iliyojazwa kwa usahihi, inayopatikana kwa watumishi, wawezeshaji jamii, na viongozi wa vikundi:- Fomu hii italipiwa baada ya kutuma maombi kiasi cha Tsh 10,000/- (elfu kumi tu) kupitia akaunti ya shirika benki ya NMB yenye jina la MTANDAO WA WAKULIMA BUNDA namba 30110004259. (Wanawake na vijana wanahamasishwa kugombea nafasi hizo)

 

Maombi yatumwe kwa;

Kamati ya Uchaguzi,

BUFADESO,

S.L.P.95,

BUNDA

 

Mwombaji atume maombi kwa sanduku la posta lililotajwa hapo juu au umpe mwezeshaji jamii au mtumishi wa BUFADESO au afikishe maombi yake katika Ofisi za BUFADESO zilizopo Sazira.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14/11/2022 saa kumi na moja jioni.

MUHURI BUFADESO.jpg

Imetolewa na

 

 

KAMATI YA UCHAGUZI

BUFADESO

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO