Maana ya Mradi:
MRADI ni mlolongo/mfululizo wa shughuli
zinazolenga kufikia lengo fulani lililo wazi ndani ya muda uliopangwa kwa
kutumia gharama zilizoainishwa.
Ni mchakato unaohusisha utoaji /uwekaji wa
rasilimali (pembejeo-inputs) kwa kipindi Fulani. Na kutumia rasilimali husika,
shughuli hutekelezwa na kuleta matokeo (results) ili kufikia lengo lililowekwa.
Ni juhudi ya pamoja katika utekelezaji kufikia lengo. Kwa
hali hiyo, mradi hautekelezwi na mtu mmoja.
Mradi unapaswa uwe na:
ü Walengwa
wanaotambuliwa: hawa wanajumuisha walengwa wa msingi (mwanzo) na walengwa wa mwisho
(jumla);
ü
Uratibu mzuri, usimamizi ulio wazi na mpangilio
bora wa kihasibu;
ü
Mfumo wa tathmini na ufuatiliaji kwa ajili ya
kufuatilia utekelezaji; na
ü
Kiwango sahihi cha uchambuzi wa kiuchumi na
gharama unaoonyesha kuwa faida za matokeo ya mradi zitakuwa kubwa/nyingi zaidi
ya gharama ya mradi.
Miradi
ya maendeleo ni njia iliyo wazi katika kuleta mabadiriko ndani ya jamii husika.
Kuna aina nyingi za miradi katika jamii kulingana na malengo, wigo, na ukubwa
wa mradi. Miradi midogo itahitaji gharama kiasi na itadumu kwa muda mfupi mfano
miezi kadhaa wakati miradi makubwa itagharimu mamilioni ya shilingi na itadumu
kwa muda wa miaka kadhaa
Mahusiano kati ya mradi, mpango (program)
na sera:
Mradi
ulioandikwa vizuri ili kufikia vipaumbele na malengo yanayotazamiwa ni lazima
uendane na mipango ya serikali pamoja na sera.
Mpango/program
ina tofauti kidogo na mradi kutokana na wigo na ukubwa. Mpango unakuwa na wigo
mpana katika utekelezaji wake, mf mpango
wa sekta ya kilimo huu unaweza kushughulikia changamoto, vikwazo, fursa
na mambo mengine mengi yanayohusu kilimo kwa mapana.
Sera
ni maelezo ya malengo na njia ya utendaji iliyochaguliwa katika kufikia malengo
husika. Sera huwekwa katika maandishi ili iwe ndio kiongozi cha maamuzi ya nini
kifanyike.
Malengo ya
mradi wowote unaofanyika katika jamii ni lazima yachangie utekelezaji wa sera
za nchi na sekta husika ili kuleta maendeleo. Wadau binafsi wanapotekeleza
mradi wanafanya kazi ili kusaidiana na serikali katika kuinua jamii.
Madhaifu ya miradi;
Miradi
katika jamii imekuwa chachu inayoleta hamasa ya maendeleo kwa jamii mbalimbali.
Hii ni kutokana na uwajibikaji katika utendaji katika kutoa elimu, na michango
mingine ya hali na mali.
Hata
hivyo, matatizo yanayotokana na masharti ya Uendeshaji kutoka kwa wafadhiri
yameleteleza mapungufu ya miradi hii mfano:
v
Jamii husika kutokuwa na umiliki wa mradi. Hii
huleta matokeo madogo ya uendelevu.
v
Miradi ya maendeleo kuwa mingi katika jamii.
Misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali wenye mikakati na mipango tofauti
ambayo hutumia gharama nyingi ambazo
hupotea wakati mwingine
Uzuri wa miradi;
v
Ushirikishwaji wa madaraka kwa jamii
v
Misaada ya dharula wakati mwingine jamii
hukumbwa na majanga ambayo serikali haiwezi kuyafanyia kazi kwa haraka, hivyo
huitaji nguvu ya ziada kutoka kwa wafadhili.
v
Huwajengea uwezo wana jamii: miradi mingi hutoa
mafunzo ya mambo mbalimbali yanayohusu jamii hivyo kuwajengea uwezo wananchi,
kuwahamashisha na kuwapa uelewa wa mambo anuai.
Mambo ya kuzingatia:
Ili mradi uwe bora na
wenye matokeo mazuri, watendaji wa mradi na walengwa wa mradi lazima wazingatie
yafuatayo:
1)
Kubadiri
mitazamo:
Mitazamo
chanya huleta uwajibikaji, mfano Uwajibikaji ili kuleta matokeo; haipaswi
kuangalia gharama tu au shughuli zitakavyofanyika. Jamii/walengwa hawapaswi
kuangalia nani ana mamlaka ya kuongoza awe mzee au kijana, mwanamke au mwanaume
kinachotakiwa kuangaliwa ni uwajibikaji wake katika kutuletea matokeo.
2)
Kubadirika
kwa majukumu na madaraka:
Katika
kuendesha mradi, kila mdau anapaswa kuwa na majukumu yake na awajibike
ipaswavyo katika kuyatekeleza.
3)
Ujuzi:
Inatakiwa
watendaji wa mradi wawe na ujuzi wa kile wanachokifanya. Inapobidi ni vizuri
wakajengewa uwezo katika nyanja za yale wanayopaswa kuyafanyia ili wayafanye
kwa ufanisi.
4)
Utaratibu
Mradi
ni lazima uwe na mfumo maalum wa kiutendaji ili kufanikisha matokeo.Utaratibu
wa kuendesha mradi lazima uwekwe katika hali inayoruhusu kuboresha na
Kuunganisha mbinu zinazoweza kufikia malengo yaliyopangwa.
Mzunguko wa
Usimamizi wa Mradi ni istilahi inayotumika kuelezea shughuli za usimamizi na
taratibu za maamuzi zitumikazo wakati wa utekelezaji wa mradi (hujumuisha
shughuli muhimu, majukumu na wajibu, nyaraka muhimu na ufanyikaji wa maamuzi).
Mzunguko
wa Usimamizi wa Mradi hufanyika kuhakikisha:
Ø
Mradi unafikia malengo makuu.
Ø
Kupima kama mradi unafaa kwa walengwa na changamoto
zilizopo.
Ø
Upembuzi yakinifu ili kubaini kama malengo
yanaweza kufikiwa kwa uhalisia.
Ø Faida
zinazopatikana kama zitakuwa endelevu.
Ili kuhakikisha mafanikio, mradi wowote unapaswa yafuatayo:
Unahitaji ushiriki hai wa wadau husika na ulenge
kukuza umiliki wa walengwa.
Uyumie mfumo wa mantiki wa programu (na mifumo
mingine) kusaidia kupima matatizo, walengwa, malengo na mikakati.
Mawasiliano na Ushirikishwaji katika kufanya maamuzi
Katika
utekelezaji wa mradi kuna awamu/hatua tano kama inavyoonekana kama Mchoro hapo
chini:
SOMO LITAENDELEA........
Limeandaliwa na Baraka Kamese
Mratibu wa Shirika - BUFADESO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni