Mabadiliko
ya tabia nchi
ni mabadiliko yanayojitokeza kwa muda
mrefu kama vile
joto,mvua nyingi au
chache ,ukame, kuongezeka kwa
hewa chafu (hewa
ya ukaa) angani.
Hali hii inasababisha
uasilia wa vitu
vilivyokuwepo kuharibika au
kupotea kabisa
VISABABISHI
Chanzo kikubwa cha mabadiriko yatabia nchi kimesababishwa na shughuli za binadamu kutokana na:
-Ongezeko la binadamu(watu)
-Uelewa mdogo (uhalibifu
wa ardhi na
uhalibifu wa misitu)
-Ufugaji
holela
-Uchomaji
moto ovyo
Ongezeko la
viwanda- na hili linachangia
zaidi.
Pamoja na
mafuta mazito ambayo
yakiungua hutoa kiasi
kikubw cha hewa
ya ukaa(co2)
SABABU ZA
UHARIBIFU WA MAZINGIRA
-Hii
husababishwa na shughuli
za kimaendeleo anazozifanya
binadamu kama vile:-
-Ukataji wa miti
katika upanuzi wa
mashamba.
-Uchomaji wa mkaa
-Biashara ya
magogo
-Ukusanyaji
wa kuni(matumizi makubwa
ya kuni)
-Shughuli za migodi
ya madini
-Ukataji miti ovyo-mbao
-Uchomaji moto
ovyo
-Mifugo mingi katika
eneo dogo
-Ukuaji wa miundo
mbinu na ongezeko
la viwanda ,mitambo pamoja
na vyombo vya
usafiri vinavyotumia dizel
-Kilimo
kisichozingatia mbinu bora
za lilimo
Kutokana na mabadiliko
hayo, matumizi haya
yakiendelea/yanapoendelea
yanapelekea:-
Ø
Kuzolota
kwa kilimo (uzalishaji
hafifu) kushamili kwa
umaskini
Ø
Milipuko
ya magonjwa
Ø
Kutokea
kw dhoruba kali
ya upepo na
kusababisha uharibifu wa mazao
na kuezuriwa kwa
nyumba /makazi ya watu
wakati mwingine hata vifo
visivyo tarajiwa(vya ghafla).
Ø
Ukame
Ø
Barafu
Ø
Tetemeko
la ardhi n.k
Ardhi-sasa
hivi ardhi yetu
imepoteza rutuba/ imechoka ,kile
unacho kusudia kukipata
hakipatikani hii ni kutokana
na kupanda mazao
kwa muda mrefu
bila kuongeza mbolea. Pia
na kutumia mbolea
za viwandani zinahalibu
ardhi yetu kwani
muda /siku ambayo
utakosa mtaji wa
kununua mbolea hizo, muda/siku
ukipanda mazao bila
kuweka mbolea hizo
za viwandani hutaweza
kuzalisha chochote.Vilevile mbolea
za viwandani na
madawa ya viwandani
yakitumika yanaua wadudu rafiki
walioko udongoni wanao
saidia kumengenya mbolea au maozea na kusababisha
ardhi isiweze kupumua vizuri (mzunguko
hafifu wa hewa
ardhini).
Misitu-
Uhalibifu wa misitu/ukataji miti
holela unasababisha uhalibifu
wa mazingira.(ardhi)
Mifugo- Mifugo inayoogeshwa
dwa zizini bila
kutumia crash, ile
dawa ikimwagika kudondoka kwenye
mbolea inaua na
kuhalibu wadudu walioko
kwenye mbolea .Hivyo
mbolea hiyo ikitumika
kupandia mazao haifanyi
vizuri kwani ile
dawa(sumu) inakuwa imeua na
kuharibu wale wadudu
ambao wangesaidia kumengenya
vizuri ile mbolea na mzunguko
wa hewa ardhini
kwenda kwa utaratibu
mzuri
Ili tuweze kujinusuru
na hali hii
yatupasa kutumia /kuchukua hatua
kuu 3 nazo
ni -1.Kusikia. 2.Kuamini. 3.Kufanya
maamuzi.
KIla mmoja
akifuata hatua hizi
tatu tunaweza kuondokana
na hali ngumu ya mabadiliko
ya tabia nchi inayo tuletea /pelekea UMASKINI
wakati muda wote
/mwingi tunaonekana tunafanya
kazi za uzalishaji
lakini tunachokizalisha hakilingani
na nguvu zetu.
MASWALI YAKUJIULIZA
*Tufanye
nini ili kuondokana
na hali hii ya
uhalibifu wa mazingira
*Ni mbinu zipi tuanze kuzitumia
katika eneo letu
ili zilete ufanisi
*Tuanze lini shughuli
hizi.
*Nimsaada
gani tupate toka
kwa wataalam
Nimahitali
gani yanahitajika ili kufanikisha
shughuli hii.
Nini kifanyike
Ili kupunguza makali
haya na sio
kuzuia kabisa lazima tutumie mbinu
endelevu za matumizi
ya ardhi ya
kilimo na mbinu hizi
endelevu zitaegemea zaidi
katika kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi katika haya
yafuatayo:-
*Mabadiliko
ya hali ya
hewa(kuongezeka kwa gesi
joto), mabadiliko makubwa ya vipindi vya
mvua ,ukame barafu na mafuriko.
*Uzalishaji
mdogo wa mazao
*Rutuba ya udongo(afya ya udongo)
*Wadudu na magonjwa
*Vyanzo vya maji
*Nishati mbadala
eg mwanga wa
jua na Biogesi
*Chakula na lishe.
MBINU ZITAKAZOTUMIKA
·
Kilimo mseto-kilimo mchanganyiko
wa mazao, miti
na mifugo
·
Kilimo
cha vijishamba vya miti
·
Matandazo-
·
Kilimo
mzunguko(mzunguko wa mazao)
·
Mifumo
rahisi ya uvunaji wa
maji ya mvua
·
Matumizi
ya mbolea itokanayo na mifugo,,mbolea za asili (mbolea vunde)
·
Mazao
funika
·
Kilimo
hifadhi(kilimo cha kutotifua
au kutifua kwa
kiasi kidogo.
·
Matumizi
ya dawa za asili
·
Ufugaji
wa ndani (ufubaji unao
kidhi)
·
Ufugaji
wa Nyuki na
ufugaji wa Samaki
kwenye mabwawa
·
Kupanda
mazao katika kontua(contour)
·
Terrace
·
Matumizi
ya mimea (miti) ya asili
inayohimili ukame
·
Mazao
yaliyo boreshwa yenye
uwezo wakuhimili wadudu
na magonjwa(mazao kinzani)
·
Umwagiliaji
·
Utumiaji
wa majiko sanifu/banifu
·
Uzalishaji
wa mkaa
·
Urutubishaji
wa udongo kwa
kutumia mabaki /masalia ya mazao mf mabua ya Mahindi,Ngano,Mtama,Viazi n.k
·
Kutumia
mbolea za kijani
·
Palizi
kwa wakati muafaka.
Mkulima akitumia
mbinu hizi hakika
ataweza
v Kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi
v Mata
asili na matokeo yake
mavuno yataongezeka
v Ataondokana na utegemezi
wa mbolea na madawa
ya viwandani
v Kuongezeka kwa
viumbe hai katika
udongo
v Kuondoa gesi
ya ukaa hewani/angani
v Atapata faida
ya ziada -
mbao na kuni.
v Atapata soko
zuri la mazao (bithaa
bora)
v Kipato kitaongezaka
(mkulima atajikwamua na
hali ngumu ya
maisha(umaskini)
v Nazaidi itasaidia
kulinda/kutunza chakula kwa
kizazi kijacho (usalama
wa chakula)
Njia kuu tano
za kufanikisha mbinu
endelevu za matumizi
ya ardhi ya
kilimo ni-
1)
Uzalishaji
wa mazao kwa wingi
na ubora
2)
Utunzaji
wa mazao
3)
Utunzaji
wa mifugo
4)
Ufanisi
wa nguvu na
matumizi ya bio-gas
na nguvu za
jua (solar)
5)
Uanzishaji
wa vitalu vya
miti
6)
Upandaji
na utunzaji wa
miti
Matandazo na
faida zake (mulching)
Matandazo -
Niufunikaji wa udongo
kwa kutumia mabaki
ya mazao au majani.Yaweza
kutumiwa shambani kabla
au baada ya
upandaji,pia na kando
kando ya mimea
ili kufunika udongo.Matandazo kwa
wastani ni mazuri
kwenye sehemu kavu
na wakati wa
misimu kavu, hata
wakati wa mvua ili
kuzuia mmomonyoko wa
udongo.
-Huongeza
mbolea(mata asili kwenye
udongo)
-Hutunza joto kwenye
udongo
-Hutunza
unyevunyevu
-Huifadhi
viumbe hai
-Huzuia
magugu kuota
-Huzuia
upotevu wa maji
-Hufanya
shamba kuwa safi(muonekano wa
shamba)
Kilimo mseto:-
Ni kilimo chamchanganyiko wa
miti na mazao
shambani yaliyopandwa kwa nafasi
maalum kitaalam ya
muda mrefu na muda
mfupi pamoja na mifugo
katika eneo moja
la shamba.
Ø
Kilimo
mseto kina uwezo
wa kustawi kwenye
udongo usio na
rutuba ,kina mizizi
ambayo huenda chini na
inauwezo wa kufikia
virutubisho kutola kwenye
tabaka la chini
la udongo bila
kushindana na mazao mengine
yaliyopandwa shambani
Ø
Virutubisho
kwenye majani ya
miti huanguka chini
na kuvunda nakuongeza
matahuruku kwenye udongo.
Ø
Husaidia
kupata mazao mbalimbali
kama vile matunda, mbogamboga,chakula,mbolea za asili, samadi, mbao na kuni,
dawa na
mengineyo.
Ø
Hushikamanisha
udongo na kuzuia mmomonyoko
wa udongo
Ø
Huifadhi
mazingira.
Mazao funika (cover
crops)
Ni mazao yanayopandwa
kwa ajili yakufunika
ardhi kama vile
Mucuna,Lablab,Canavalia, Desmodium,Tephrosia, Sesbania Mbaazi n.k
-Huifadhi
udongo kwa sababu
hufunika ardhi
-Huzuia
mmomonyoko wa udongo
.
-Huzuia magugu
.Huzuia sura ya
udongo.
-Huongeza
rutuba ya udongo.
-Hutunza
unyevunyevu.
-Huzuia maji kutiririkaovyo na hutunza
maji yasipotee hewani.
-Hutupatia kuni,dawa nanyingine
malisho ya mifugo
-Mengine
hutupatia chakula kam
mbaazi
Mbolea vunde
(compost manure)
Mbolea vunde ni
limbukizo la mbolea /takataka / masalia ya mazao
na mimea iliyo
kusanywa kwenye mashimo
zikivundwa /kuoza zaweza
kutengenezwa kwa kutumia
vitu kama hivyo
na kutoa mbolea
vunde, na kutoa virutubisho kwa
mimea /Mbolea vunde
hutengenezwa kwa kuozesha
takataka mbalimbali kama
vile magugu na
maganda ya mazao ya
chakula (ndizi, maharage,viazi vitamu
Alizeti pori n.k )
vitu
hivyo vinachanganywa na
majivu, nyasi kavu kinyesi
cha mifugo na udongo. Vitu
vilivyo vundikwa vinaweza kuongeza rutuba
katika udongo wa
aina tofauti.
Uwezo wa udongo
kutoa virutubisho hupungua
kadri tunavyoendelea kustawisha
mazao. Hivyo ni lazima
kutumia juhudi na
maarifa ili kuboresha
na kudumisha virutubisho
vya mimea kwenye
mashamba yetu
Nanjia
mojawapo yakufanya hivyo nikutengeneza mbolea
vunde/ mboji.
Faida ya mbolea
vunde/mboji
Ø
Gharama
yake ni ndogo
kuliko aina nyingine
za mbolea
Ø
Huboresha /hurutubisha vizuri hali ya
udongo na kukaa
muda mrefu zaidi
kuliko mboea za
viwandani.
Ø
Huboresha
sura ya udongo
Ø
Hutengenezwa
kwa urahisi
Ø
Hutunza
vizuri viumbe hai
Ø
Huboresha
mzunguko mzuri wa
hewa kwenye udongo
Ø
Huchanganyikana
na udongo bila
kuachana
Ø
Hurutubisha
mimea haraka
Ø
Huboresha
ladha ya chakula (Bidhaa bora katika
soko la Kimataifa na
soko letu kwa
ujumla) na kulinda afya
zetu.
Kilimo mchanganyiko(Intercropping)
Ni kilimo kinacholimwa
kwa kuchanganya mazao mawili
au zaidi kwa
mistari katika eneo
moja la shamba /kwa msimu au
wakati mmoja
Mbinu hii
husaidia kuboresha udongo
ikiwa umetumia/umepanda mazao
yanayotoa mbolea ardhini
na yanayoingiza mbolea
ardhini/udongoni.
Mf mahindi na
maharage karanga na viazi
vitamu
Mbolea za
wanyama
Ni kinyesi cha
wanyama ambacho hukusanywa
kwa urahisi kutoka
kwenye banda (zizi) ufugaji
wa ndani na
kuvundikwa moja kwa
moja kwa kufunikwa
na majani/nyasi kavu
kabla ya kusambazwa
shambani kwa muda
wa miezi mitatu
Wanyama ambao hupata
malisho bora hutoa
mbolea yenye virutubisho
vingi zaidi kama
vile calliandra,Lusina, Desmodium,
Sesbania n.k
Huboresha mazao, huunganisha udongo ,huifadhi kiasi
cha maji kwanye
udongo
Huongeza
upenyaji wa maji
kwenye undongo
Kontua
(contour and terrace)
Kontua ni mitalu
inayolimwa /chimbwa kufuatana
au kulingana na
hali halisi ya
mteremko kwa kutumia
vipimo maalum (A-frame na mambo)
na kuweka alama
katika eneo lenye
mteremko . Na
hiyo A-frame ni
vema itumike wakati
wa kiangazi ambapo
ardhi inakuwa ngumu/imegandamizwa hivyo
miguu ya A-frame
haididimii katika udongo
.
Mtalu huo ukisha
chimbwa au kulimwa
unasaidia kuzuia mmomonyoko
wa udongo, kuzuia maji ili yasipotee/yasitiririke haraka
na nakupoteza au
kusomba virutubisho kutoka
eneo husika
Hutunza maji na
kulishia shamba taratibu
Huzuia virutubisho kupotea
toka eneo husika
Palizi
Ni tendo la
kuondoa magugu shambani
na kuweka mazao
katika hali nzuri.
Hupunguza
ushindani wa ufyonzaji
wa virutubisho na
maji toka shambani
Husaidia
kupunguza wadudu na
magonjwa shambani
Hulifanya
shamba kuwa na muonekano
mzuri (shamba kuwa safi)
Kuna njia mbili
za kuondoa magugu
shambani-
1.Palizi kwa
kutumia jembe au
mikono
2.Palizi lakutumia
madawa ya viwandani
na njia hii sio
nzuri kwani ikitumika
inaua wadudu marafiki
mashambani.
UTUNZAJI MAZINGIRA
KWA KUTUMIA MAJIKO
SANIFU
Utumiaji wa majiko
sanifu / banifu
kwa jamii kwa
lengo la kutunza
mazingira.
Majiko sanifu lengo
lake ni kubana
matumizi ya kuni
kwa kutumia kuni/mkaa
kidogo ili kupunguza
ukataji miti ovyo,kuwa
na uoto wa
asili na kuwa na
misitu ya kutosha
katika jamii zetu .Pia
kuwa na uwezekano
mzuri wa kutunza
mazingira na kuepukana
na jangwa kama
ilivyo sehemu nyingine
hapa nchini na
Afrika kwa ujumla
Elimu duni inafanya
jamii zetu kuwa
na uchangiaji mkubwa
wa uharibifu wa
mazingira hasa kwa
nchi yetu Tanzania.
Kutokana na hali
hii Tanzania kupitia
mashirika mbalimbali na
serikali kwa ujumla
imekuwa imeanzisha mkakati
mahususi wa kutoa
elimu kwa jamii
zetu kuhusu utunzaji
wa mazingira.
Kwa kutumia mbinu
endelevu za kilimo
na hii ni
pamoja na utengenezaji/utumiaji wa
majiko sanifu/banifu ili
kusaidia /kujinusuru na
wimbi la umaskini
na kuwa wajasiliamali
wazuri kwa kutumia rasilimali tulizo
nazo, kufanya mazingira
kuwa masafi na
endelevu, kutunza raslimali
zilizopo kwa ajili ya kizazi
kijacho .
Mazingira ni mambo
yote yaliyomzunguka binadamu
ambayo ni viumbe
hai na visivyo
hai
UTENGENEZAJI WA MBOLEA
VUNDE
Kuna njia mbili zakutengeneza
mbolea vunde /mboji
1.Kutengeneza kwa kutumia
mlundo
2.Kutengeneza kwa kutumia
shimo
Njia zote mbili
hutumiwa kwa kufuatana
nahali ya hewa
ya mahali ulipo.
-Sehemu zenye mvua
nyingi na mvua za kadri,
tumia njia ya
mlundo
Njia hii
hupunguza unyevu nakulifanya
lundo liweze kuoza
vizuri.
Sehemu
zenye mvua kidogo
tumia njia ya
shimo.
Njia hii
hutunza unyevu ili
lundo liweze kuoza
vizuri
Hatua za
utengenezaji wa mbolea
vunde/ mboji
§
Tayalisha
vifaa vifuatvyo:-Jembe,vifaa
vyakuchotea maji,kijiti chakupimia
joto, nguzo,nyasi/majani, mabua
ya mahindi, majivu
samadi na udongo
§
Pima
eneo lenye urefu
wa meta 2
na upana wa
meta 2 mraba
§
Simika
nguzo kila pembe
ya eneo
§
Jenga
tabaka lakwanza la
mabua makavu / nyasi
kavu kama huna
mabua ya mahindi
sentimeta 10-15 unene.
§
Kama
umepata mabua juu
ongezea nyasi kavu
§
Jenga
tabaka la samadi
/kinyesi cha mifugo
sm 5 - 10
§
Weka juu udongo
kidogo sm 2
§
Ongeza
tabaka la takataka,
masalia ya mazao
n.k hili ndilo
tabaka kubwa sana
kuliko zote litakalo
unda sehemu kubwa
ya mbolea, unene
sm 15.
§
Mwagilia
maji yakutosha ili
tabaka zote zipate
unyevu ziweze kuoza
vizuri.
§
Juu
weka tabaka la
majivu kusaidia uvundaji/uozaji wa
tabaka nyingine sentimeta
2
§
Jenga
tabaka la samadi / kinyesi cha
mifugo sm 5-10
§
Fanya
hivyo kila baada
ya tabaka la
udongo
§
Rudia
mpangilio huu kuanzia
na nyasi kavu
mpaka lundo lifikie
kimo cha meta
1.5
§
Baada
ya kufikia kimo
hicho lundo lifunikwe
kwa nyasi au
magunia au mikeka
iliyo chakaa.n.k
§
Juu
kabisa ya lundo
jenga kivuli ili
mvua na jua
visiharibu ubora wa
mbolea
§
Lundo
ligeuzwe kila baada ya
majuma matatu ili
tabaka zilizo chini ziwe
juu na za
juu ziwe chini
kwakuhamishia eneo lingine.
§
Kata
kijiti kirefu kasha
kichomeke katikati ya
lundo, Hiki kitakusaidia
kupima joto nakuangalia mbelea
kama inaendelea kuoza
vizuri (unyevunyevu wakutosha)
Mambo muhimu
ya kuzingatia
*Ujenzi wa lundo
ukamilike kwq siku
moja tu
*Chomoa kijiti kila
baada ya siku
nne ili kupima
joto la lundo
*Iwapo lundo
halina joto la
juu fahamu kuwa
halijaoza
*Ikiwa uozaji
umekwenda vizuri mbolea
itakuwa tayari baada
ya miezi miwili
hadi mitatu
*Tengeneza mboji/mbolea vunde
nyingi kwenye musimu
wa mvua
Kilimo mzunguko /
mzunguko wa mazao (crop
rotation)
Kilimo mzunguko
ni kilimo kizuri
sana kwani kinasaidia
-Kuzuia
wadudu waharibifu wa
mazao, magugu na magonjwa.
-Pia kilimo hiki
husaidia kuongeza mbolea
kwenye udongo kwani unapopanda mazao
yanayotoa mbolea na musimu
unaofuata/mwingine unapanda mazao
yanayoongeza/ ingiza mbolea ardhini
mf ukipanda mahindi
na baadae musimu
unofuata unapanda maharage
au karanga.
Mbolea za
kijani (Green manure )
-Ni mimea au
miche inayopandwa kwa
madhumuni ya kufunikawa
/kutifuliwa kwenye
udongo ili kuongeza
mbolea /virutubisho zaidi kwenye
udongo
- Ni mimea
inayopenyeza / ingiza Nitrogen
kwenye udongo (sana sana mikunde
kunde)
-Mimea hii hukua
haraka,hufunika ardhi (udongo)
-Huzuia
mmomonyoko wa udongo
-Mbolea hii husaidia
maji kupenya kwa
urahisi
-Huzuia
magugu kuota
-Hupunguza
magonjwa na nematode
-Nichimbuko
la malisho ya
mifugo
-Mimea
mingine huzalisha chakula
cha binadamu
-Haitumii
nguvu kazi nyingi
-ni nzuri kwa
udongo usio na
rutuba na mkavu.
TUMIA MBINU HIZI
KWA KUTUNZA MAZINGIRA,
NA KABILIANA NA MABADILIKO
YA TABIA NCHI
Imeandaliwa na BARAKA KAMESE
Mratibu - BUFADESO
Mratibu - BUFADESO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni