TANGAZO LA AJIRA YA
AFISA MRADI
Bunda Farmers Development Support
Organization (BUFADESO) ni shirika lisilokuwa la kiserikali linalofanya kazi
wilayani Bunda, Mara-TANZANIA. Shirika la BUFADESO lilianzishwa tarehe
27/02/2012 na limesajiliwa tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696
chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya
kiserikali. Mpaka sasa shirika la BUFADESO lina wanachama vikundi 112 kutoka
kata za Neruma,
Guta, Hunyari, Mcharo, Nyamang`uta, Kabasa, Nyamuswa, Sazira, Wariku, Ketare
na Kunzugu.
DIRA YETU:
Kuwa asasi imara
yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda.
DHAMIRA YETU:
Kujengea
uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu.
Shirika la BUFADESO linakaribisha maombi ya ajira kwa
nafasi ya AFISA MRADI kwa watanzania
wenye sifa, na uwezo.
KITUO CHA KAZI: Wilaya ya Bunda
MUDA WA KAZI: Mkataba wa mwaka mmoja. Muda wa mkataba wa ajira unaweza kuongezwa kutokana na utendaji wa mtumishi.
KITUO CHA KAZI: Wilaya ya Bunda
MUDA WA KAZI: Mkataba wa mwaka mmoja. Muda wa mkataba wa ajira unaweza kuongezwa kutokana na utendaji wa mtumishi.
MAJUKUMU YA AFISA MRADI:
Afisa Mradi wa
shirika la BUFADESO atatekeleza majukumu yafuatayo:
1.
Kusimamia
utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendeshwa ya shirika kwa kuzingatia
bajeti na mipango kazi.
2.
Kutoa
elimu na mafunzo ya mambo yanayohusu kilimo mseto, Kilimo biashara, Mabadiriko
ya Tabia Nchi, Nishati Mbadala, Mazingira, Ujasiriamali, Usawa wa Kijinsia na
mada nyingine zinazowalenga wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali.
3.
Kutoa
mafunzo ya vitendo ya kilimo na ufugaji.
4.
Kufuatilia
maendeleo ya vikundi wanachama wa shirika.
5.
Kusimamia
vikao na mikutano ya vikundi wanachama na kutoa miongozo na maelekezo.
6.
Kuhamasisha
vikundi vya wakulima na wafugaji masuala mtambuka.
7.
Kujengea
uwezo jamii katika utekelezaji wa shughuli walizopanga.
8.
Kutengeneza
mahusiano mazuri kati ya shirika, jamii, vikundi, asasi mbalimbali na serikali
ili kufanikisha shughuli za maendeleo.
9.
Kuwajengea
uwezo viongozi wa vikundi na wawezeshaji jamii katika kutekeleza shughuli zenye
kuleta maendeleo endelevu.
10. Kuhamasisha na
kufundisha shughuli za kuongeza kipato halali kwa jamii.
11. Kuwezesha uanzishwaji
na uendelevu wa vikundi
12. Kuwakilisha shirika
kwa Washika dau mbalimbali.
13. Kupanga, kutekeleza
na kufuatilia shughuli za kila siku za vikundi wanachama.
14. Kutunza kumbukumbu za
shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikundi wanachama na shirika.
15. Kutekeleza majukumu
mengine anayopewa na Msimamizi wake au uongozi wa Shirika,
SIFA
ZA MWOMBAJI:
1. Awe
Mtanzania.
2. Awe
na astashahada/stashahada ya masomo ya Kilimo/Mifugo/Mazingira/ Maendeleo ya
Jamii kutoka chuo kinachotambulika na serikali ya Tanzania.
3. Awe
na ujuzi wa kutumia kompyuta.
4. Awe
muaminifu na muadilifu.
5. Awe
anajua kuendesha pikipiki na mwenye leseni ya udereva (Daraja A)
6. Awe
tayari kufanya kazi katika maeneo ya vijijini. Shirika la BUFADESO linafanya
kazi na jamii ya wakulima na wafugaji wanaopatikana maeneo ya vijijini.
Asilimia sabini na tano (75%) ya majukumu ya Afisa Mradi yatafanyikia maeneo ya
vijijini walipo wanachama.
MUDA
WA MKATABA:
Afisa Mradi wa Shirika atafanya kazi kwa Mkataba wa mwaka
mmoja mmoja. Mkataba wa ajira unaweza kuongezwa kutokana na utendaji kazi wa
mtumishi.
Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma
pamoja na taarifa binafsi (C.V) na ziwasilishwe kwa barua pepe au kupitia posta.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 2 Januari 2017
Maombi yatumwe kwa;
Mwenyekiti,
Bunda Farmers
Development Support Organization,
BUFADESO,
S.L.P. 95,
Bunda,
Mara - TANZANIA.
Limetolewa na;
BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA
BUFADESO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni