Jumatano, 21 Desemba 2016

TANGAZO LA AJIRA YA MUDA NAFASI YA MHASIBU

TANGAZO LA AJIRA YA MUDA NAFASI YA MHASIBU
(TEMPORARY ACCOUNTANT EMPLOYMENT)

Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO) ni shirika lisilokuwa la kiserikali linalofanya kazi wilayani Bunda, Mara-TANZANIA. Shirika la BUFADESO lilianzishwa tarehe 27/02/2012 na limesajiliwa tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696 chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya kiserikali. Mpaka sasa shirika la BUFADESO lina wanachama vikundi 112 kutoka kata za Neruma, Guta, Hunyari, Mcharo, Nyamang`uta, Kabasa, Nyamuswa, Sazira, Wariku, Ketare na Kunzugu. 

DIRA YETU:                                                                                                                          
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda.

DHAMIRA   YETU:                                                                                                                              
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu.
Shirika la BUFADESO linakaribisha maombi ya ajira ya muda kwa nafasi ya MHASIBU kwa watanzania wenye sifa, na uwezo.

KITUO CHA KAZI: Wilaya ya Bunda

MAJUKUMU YA MHASIBU:
Mhasibu wa shirika la BUFADESO atatekeleza majukumu yafuatayo:
1.    Ataandika na kutunza vitabu vya mahesabu na kumbukumbu nyingine.
2.    Atapokea fedha yote inayoingia katika shirika na kufanya malinganisho ya fedha inayopokelewa na inayolipwa kila siku.
3.    Kufanya malinganisho ya hesabu za benki kila mwezi na kufanya ulinganisho wa fedha mkononi/kwenye kasiki kila siku.
4.    Kufanya masawazisho ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuandaa hesabu ya mapato na matumizi ya mwaka.
5.    Kutayarisha taarifa kila mwezi, hesabu ya mapato na matumizi na kuiwasilisha kwa Mratibu pia atatoa ripoti ya kila robo mwaka (miezi mitatu) kwenye vikao vya Bodi.
6.    Kusaidia ukaguzi wa hesabu unaofanywa na wakaguzi.
7.    Ataandaa ripoti ya matumizi ya fedha kwa wafadhiri kila mwezi.
8.    Atasaidiana na viongozi wa shirika kufanya shughuli yoyote inayohusiana na fedha na mahesabu ya shirika.

SIFA ZA MWOMBAJI:
1.    Awe Mtanzania.
2.    Awe na astashahada/stashahada ya masomo ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambulika na serikali ya Tanzania.
3.    Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
4.    Awe muaminifu na muadilifu.
Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma pamoja na taarifa binafsi (C.V) na ziwasilishwe kwa barua pepe au kupitia posta. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 2 Januari 2017
Maombi yatumwe kwa;
Mwenyekiti,
Bunda Farmers Development Support Organization,
BUFADESO,
S.L.P. 95,
Bunda,
Mara - TANZANIA.
Barua pepe: bufadeso@gmail.com

Limetolewa na;
BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA
BUFADESO
  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO