Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Africa.
Shirika la BUFADESO linaungana kuadhimisha siku hii kwani linatambua mchango wa watoto katika kuleta maendeleo hasa katika sekta ya kilimo na mazingira. BUFADESO pia hushirikisha watoto katika shughuli na miradi mbalimbali ambapo kupitia watoto elimu ya utunzaji mazingira mashuleni hutolewa.
BUFADESO inaamini watoto ni WAKULIMA WA BAADAE. Pichani ni mtoto akipanda mti kwa ajili ya kuboresha mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni