Jumatano, 10 Mei 2017

UONGOZI WA MABADIRIKO


UONGOZI ni mahusiano ya kuhamasisha kati ya kiongozi na watu anaowaongoza; kiongozi lazima ajue mabadiriko yanayokusudiwa na Matokeo yanayohitajika kutokana na malengo.
Uongozi ni
Ushirikiano kati ya viongozi na wafuasi (wanaoongozwa).
Mahusiano mazuri na kujenga hamasa.
Usitawaliwe na matakwa binafsi (umimi).
Kuangalia mbele (kulenga maendeleo/ kukua/ kukomaa)
Kusimamia malengo (kuendeshwa na dhumuni)

UONGOZI WA MABADIRIKO ni aina ya uongozi inayolenga kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kupitia uwajibikaji wa dira/ndoto/maono.
MABADIRIKO NI NINI?
Ni kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
-Mabadiriko yanaanza na mtu mmoja.
-Mtu huyu anaamua kuwa mshindi (mwanamapinduzi) wa Kufanikisha malengo.
-Mshindi huyu anahamasisha watu wachache anaofanya nao kazi (sio kuhamasisha washindi wengine)
-Mshindi huyu anatafuta njia za kupanua wigo na ushawishi na kusambaza wazo la hitaji la mabadiriko katika jamii.

TABIA ZA KIONGOZI ANAYETAKA KULETA MABADIRIKO:
Anajifunza: anatafuta mawazo mapya, maoni tofauti na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali.
Ana hamasa: ana shauku ya mafanikio kiasi cha kuamsha hisia na mitazamo ya wengine.
Anajitambua: anachukua muda kuvumilia changamoto na kupitia hatua za maumivu ili kukomaa kifikra.
Anaona mbali: anaweza kufaulu na kukua. Anataka watu wake wawe mbele (Sisi tuongoze: wengine wafuate)
Ana husudu mabadiriko: anapenda kuwa wakala wa mabadiriko kwa watu anaowaongoza, wapate mafanikio kupitia uongozi wake.
Ni tabibu: anahamasisha na kutuliza hisia za watu wenye mawazo hasi. Anageuza mitazamo inayowaza  kushindwa na kuifanya ione mafanikio yaliyopo mbele.
Anapenda Umoja: anajenga mahusiano mazuri. Anawaunganisha watu wawe kitu kimoja.
Anajua kuwasiliana: anawaeleza wafuasi wake kinachojiri katika mchakato wa maendeleo (mafanikio na vikwazo vilivyopo, pamoja na njia ya kutatua changamoto ili kufikia malengo)
Ni mtumwa: anafanya kwa ajili ya wengine. Anatoa sadaka rasilimali zake ili Kufanikisha malengo.

HATUA ZA UONGOZI WA MABADIRIKO:
Uongozi wa mabadiriko unapitia hatua tatu:
1. Mtu Binafsi: nafsi ya kiongozi mwenyewe.
2. Baadhi ya watu: walio karibu na kiongozi.
3. Jamii: Walengwa katika eneo husika.
1. MABADIRIKO YA MTU BINAFSI (KIONGOZI)
Wewe kama kiongozi jiulize maswali yafuatayo:-
a) Mimi ni nani kama mtu na kama kiongozi?   (Jifanyie tathmini ya UUNATI)
b) Mimi ni kiongozi wa aina gani?: Dikteta, kidemokrasia, mtumwa, mbunifu, mhamasishaji, mzalendo au kiongozi hali?
c) Watu ninao waongoza wananionaje (wananichukuliaje) na nina husianaje na mimi ninavyo jichukulia (ninavyo jifikiria)?
d) Je, mawazo/fikra zangu zipo katika hatua gani ya mabadiriko?
e) Nina elewa (nina tambua) mahusiano yangu katika uongozi wangu?

Mfano: 
Yai                                                                                                         
 -Limetulia muda wote                        
 -Halidhuru              
 -Ni rahisi kuliharibu                                        
 -Halielewi mazingira            
  -Halili                                        
  -Halizalishi                       
  -Linapendwa                                      

Duduwasha
-Linatembea muda wote
 -Linadhuru
  -Linaogopesha
  -Linatafuta
-Linakula sana
  -Linazalisha
 -Linachukiwa

Kipepeo
 -Kinazunguka muda wote
-Kinaweza kudhuru
 -Kinavutia
 -Ni rahisi kukiona
-Hakili sana
 -Kinazalisha
 -Kinapendwa sana

Kiongozi lazima ujue changamoto gani “zinafunga” ubongo/mawazo yako. Yaweza kuwa familia, mila, dini, elimu, jinsia, au kipato chako.
Kubadirisha mtazamo wako; wewe kama kiongozi; jipangie mabadiriko binafsi ya muhimu:- tengeneza mpango wako wa mafanikio yako.
Nataka kwenda wapi?
(MALENGO) Vitu gani vizuri ninavyo
Niviendeleze?
(UWEZO)
Mambo gani siyahitaji?
(UDHAIFU) Kina nani watatembea nani?
(NAFASI)
Kauli mbiu ya Maisha yako ni nini?

2. MABADIRIKO YA JAMII
Zingatia usawa
Zingatia ujumuishaji
Nenda hatua kwa hatua kwa Sababu mabadiriko ni mchakato.
                 Onyesha umuhimu
                 Tengeneza kikosi kazi (timu)
                 Weka dira
                 Fanya mawasiliano kuhamasisha sawa
Tekeleza mpango kazi
                Tengeneza mafanikio ya muda mfupi
                Usikate tamaa
                Kazana
                                                     
Yameandaliwa na Baraka Kamese                                                                               

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO