Maafisa wa idara za Halmashauri za Wilaya na Mji Bunda kstiks uzinduzi huo |
Tunaamini burudani ni njia mojawapo ya kufikishwa ujumbe
katika jamii, hivyo kupitia burudani BUFADESO imeona fursa ya Kuelimisha na
kuhamasisha jamii juu ya Usawa wa jinsia na kupinga ukatili wa jinsia.
Tunaamini kupitia mradi huu unao zinduliwa leo, jamii itapata fursa sio tu kuburudika
kupitia burudani zilizo andaliwa bali kupata ujumbe na mwisho wa siku
kubadirika na kuacha matendo yanayokiuka utu wa mwanamke. Vikundi wanachama wa
BUFADESO vimeandaa Nyimbo na ngoma za kiutamaduni au kikabila zenye ujumbe
nzuri unaohamasisha usawa wa jinsia. Nyimbo hizo zinajumuisha Nyimbo za kabila
la Wakurya maarufu kama Litungu. Nyimbo za kabila la Waikizu zijulikanazo kama
Ndono, Kesa na Bwenga. Nyimbo za Wasukuma Masaligula na Kadumu pamoja na kwaya
zenye maudhui ya usawa wa jinsia.
Baada ya Uzinduzi huu, BUFADESO itazunguka katika kata 11 za
wilaya ya Bunda tunapofanyia kazi ili kuendeleza kuhamasisha jamii juu ya Usawa
wa Jinsia. Pamoja na kuzunguka katika maeneo hayo tofauti, tunaomba ushirikiano
wa vyombo vya habari katika kutumia Nyimbo na ngoma hizi zilizo andaliwa ili
kuhamasisha jamii juu ya jambo hili. Pia tunaomba serikali iendelee kutia mkazo
na kutumia sheria juu ya wananchi wanaoendeleza matendo ya unyanyasaji wa
jinsia. Mbali na hayo tuna waasa Wanajamii kutoa taarifa kwenye vyombo husika
pale wanapofanyiwa au kuona mwananchi anafanya matendo ya unyanyasaji wa
jinsia.
Mwisho kabisa tunaomba na kutoa hamasa kwa jamii hasa watu
waliopo vijiji tofauti vya wilaya hii ya Bunda kuacha matendo yote yanayo husiana
na kunyanyasa na kukandamiza wanawake na hivyo kusababisha wilaya yetu na mkoa
wa Mara kwa ujumla kuwa maarufu kwa sifa mbaya ya Unyanyasaji wa Wanawake.
BUFADESO tunaamini kuwa katika familia na jamii yoyote haiwezi kupata maendeleo
endapo hakuna ushiriki wa wanawake. Bila ushiriki wa wanawake kuanzia ngazi ya
familia shughuli hazitafanyika kwa weledi. Wakulima hawawezi kunufaika na
kilimo iwapo mwanamke hapewi fursa ya kushiriki katika shughuli za kutoa
maamuzi na mawazo ya kuendeleza kilimo cha familia, hiyo pia haiwezekani katika
shughuli za kibiashara, hata katika nyanja ya uongozi; haiwezekani kuwa na
ufanisi endapo mwanamke atanyimwa fursa na haki zote anazo stahiki.
Akizindua mradi huu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili ameilezea jamii kuwa yeye ni mdau mkubwa wa kupinga ukatili wa jinsia. Aidha aliwaasa wananchi kuachana na "mambo ya kale" ya kunyanyasana kwani ni mambo yaliyopitwa na wakati na husababisha kudolola kwa uchumi. Mkuu huyo wa wilaya aliwasisitiza wanacnhi kuachana na mfumo dume na kufanya kazi kwa pamoja. Zaidi aligusia pande zote kuwa wanaonyanyaswa kijinsia sio tu wanawake bali pia wapo wanaume wanaoyanyasika kijinsia na wake zao. Mkuu wa wilaya hii ya Bunda alilipongeza shirika la BUFADESO kwa utekelezaji mzuri wa shughuli zake ikiwemo ya kuhamasisha jamii juu ya usawa wa jinsia.
Mkuu wa wilaya na viongozi wa BUFADESO wakifurahia burudani na ujumbe kutoka ngoma za kikabila |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni