Vi Agroforestry Tanzania inapenda kuwaalika wadau wote
kwenye kongamano la maonesho ya shughuli za kilimo mseto litakalofanyika
kuanzia tarehe 22 hadi 24, November. Maonesho yatafanyika katika kituo cha
mafunzo ya kilimo kilichopo Bweri katika Manispaa ya Musoma kuanzia saa tatu
asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Wanaoalikwa kuhudhuria kongamano hilo ni pamoja na
vikundi vya wakulima wadogowadogo, makampuni ya uzalishaji na utengenezaji wa
bidhaa mbalimbali, makampuni ya mbegu, makampuni yanayo zalisha viuatilifu,
taasisi za fedha, taasisi za elimu, viwanda vya nguo, wizara na taasisi za
serikali, taasisi za utafiti pamoja na taasisi za afya na bima na wengine wote
watakaopata nafasi.
Kongamano hilo litajumuisha maonesho ya tekinolojia
mbalimbali za kilimo, huduma na bidhaa za kilimo kwa kuzingatia utaratibu
utakaowekwa na waandaaji.
Mazingira endelevu ni agenda ya kudumu ya Taasisi yetu.
Katika maonesho hayo pia kutakuwepo na mafunzo mbalimbali yatakayotolewa na
wadau na wakulima washiriki yatakayo toa fursa ya kujifunza na kupata maarifa
mapya kwa mstakabali mwema wa mazingira yetu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Tunapenda kuwahahakishia ushirikiano wetu katika
mwendelezo wa utoaji wa elimu endelevu, uzoefu, technologia na mawasiliano
katika kuhakikisha kilimo na mazingira endelevu vinadumishwa. Ratiba nzima
itakolezwa na vikundi kadhaa vya burudani vitakuwepo kutoa burudani.
Kauli mbiu ya
maonyesho ya mwaka huu ni “Kilimo Mseto kwa Maendeleo ya Viwanda” zalisha kwa
tija kufikia maendeleo endelevu.
Kwa mawasiliano zaidi juu ya kongamano la mwaka huu
tafadhali wasiliana na Mratibu wa kongamano kwa kutumia Email james.juma@viagroforestry.org ama namba ya simu 0786-648000/0759070182.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni