Ijumaa, 8 Machi 2019

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

"BADIRI FIKRA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA KWA MAENDELEO ENDELEVU"
Image may contain: one or more people and crowd
Katika Picha, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwl. Lydia S. Bupilipili akikagua shughuli za kijasiriamali zinazofanywa na wanawake wa wilaya ya Bunda. Kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa inalenga kubadiri fikra kwa wanajamii ili waweze kumthamini mwanamke kuwa anaweza kufanya kama mwanaume. Hivyo basi jamii inasisitizwa kuzingatia usawa wa kijinsia kuanzia fursa, matumizi ya rasilimali na muda. Tukiwapa wanawake na wanaume fursa sawa, itakuwa chachu kubwa ya kufikia maendeleo endelevu.

Na:
Baraka Kamese

Ijumaa, 1 Februari 2019

TAARIFA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

Kaimu Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anapenda kuyakumbusha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuwasilisha Taarifa za mwaka 2018 kwa mujibu wa kifungu Na. 29 (a) & (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 na Kanuni Na. 10 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 (GN 152, 2004) kama ilivyorekebishwa na Kanuni Na. 6 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2014 (GN 8, 2015), kabla ya tarehe 15 Aprili, 2019. Taarifa hiyo ijumuishe Taarifa za utendaji kazi, Taarifa za fedha zilizokaguliwa, NGO Fomu Na. 10 na malipo ya ada ya mwaka. Mashirika yatakayoshindwa kutekeleza agizo hili ndani ya kipindi husika, yatachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.

Ijumaa, 16 Novemba 2018

Kongamano la Mwaka kwa Wadau wa Kilimo-Mseto-2018


Vi Agroforestry Tanzania inapenda kuwaalika wadau wote kwenye kongamano la maonesho ya shughuli za kilimo mseto litakalofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24, November. Maonesho yatafanyika katika kituo cha mafunzo ya kilimo kilichopo Bweri katika Manispaa ya Musoma kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Wanaoalikwa kuhudhuria kongamano hilo ni pamoja na vikundi vya wakulima wadogowadogo, makampuni ya uzalishaji na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali, makampuni ya mbegu, makampuni yanayo zalisha viuatilifu, taasisi za fedha, taasisi za elimu, viwanda vya nguo, wizara na taasisi za serikali, taasisi za utafiti pamoja na taasisi za afya na bima na wengine wote watakaopata nafasi.

Kongamano hilo litajumuisha maonesho ya tekinolojia mbalimbali za kilimo, huduma na bidhaa za kilimo kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na waandaaji.

Mazingira endelevu ni agenda ya kudumu ya Taasisi yetu. Katika maonesho hayo pia kutakuwepo na mafunzo mbalimbali yatakayotolewa na wadau na wakulima washiriki yatakayo toa fursa ya kujifunza na kupata maarifa mapya kwa mstakabali mwema wa mazingira yetu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Tunapenda kuwahahakishia ushirikiano wetu katika mwendelezo wa utoaji wa elimu endelevu, uzoefu, technologia na mawasiliano katika kuhakikisha kilimo na mazingira endelevu vinadumishwa. Ratiba nzima itakolezwa na vikundi kadhaa vya burudani vitakuwepo kutoa burudani.

Kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni “Kilimo Mseto kwa Maendeleo ya Viwanda” zalisha kwa tija kufikia maendeleo endelevu.

Kwa mawasiliano zaidi juu ya kongamano la mwaka huu tafadhali wasiliana na Mratibu wa kongamano kwa kutumia Email james.juma@viagroforestry.org ama namba ya simu 0786-648000/0759070182.


Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO