Jumamosi, 23 Desemba 2017

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

NAFASI YA AFISA MRADI
Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO) ni shirika lisilokuwa la kiserikali linalofanya kazi wilayani Bunda, Mara-TANZANIA. Shirika la BUFADESO lilianzishwa tarehe 27/02/2012 na limesajiliwa tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696 chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya kiserikali. 
DIRA YETU:
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda.
DHAMIRA YETU:
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu.

Shirika la BUFADESO linakaribisha maombi ya ajira kwa watanzania wenye sifa, na uwezo wa kujaza nafasi ya AFISA MRADI wa shirika hili.

MAJUKUMU YA AFISA MRADI:
Afisa Mradi wa shirika la BUFADESO atatekeleza majukumu yafuatayo:
1.      Utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendeshwa ya shirika kwa kuzingatia bajeti na mipango kazi.
2.      Kutoa elimu na mafunzo ya mambo yanayohusu kilimo mseto, Kilimo biashara, Mabadiriko ya Tabia Nchi, Nishati Endelevu, Mazingira, Ujasiriamali, Usawa wa Kijinsia na mada nyingine zinazowalenga wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali.
3.      Kutoa mafunzo ya vitendo ya kilimo na ufugaji.
4.      Kufuatilia maendeleo ya vikundi wanachama wa shirika.
5.      Kusimamia vikao na mikutano ya vikundi wanachama na kutoa miongozo na maelekezo.
6.      Kuhamasisha vikundi vya wakulima na wafugaji masuala mtambuka.
7.      Kujengea uwezo jamii katika utekelezaji wa shughuli walizopanga.
8.      Kutengeneza mahusiano mazuri kati ya shirika, jamii, vikundi, asasi mbalimbali na serikali ili kufanikisha shughuli za maendeleo.
9.      Kuwajengea uwezo viongozi wa vikundi na wawezeshaji jamii katika kutekeleza shughuli zenye kuleta maendeleo endelevu.
10.  Kuhamasisha na kufundisha shughuli za kuongeza kipato halali kwa jamii.
11.   Kuwezesha uanzishwaji na uendelevu wa vikundi
12.  Kuwakilisha shirika kwa Washika dau mbalimbali.
13.  Kupanga, kutekeleza na kufuatilia shughuli za kila siku za vikundi wanachama.
14.  Kutunza kumbukumbu za shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikundi wanachama na shirika.
15.  Kutekeleza majukumu mengine anayopewa na Msimamizi wake au uongozi wa Shirika,

SIFA ZA MWOMBAJI:
1.      Awe Mtanzania.
2.      Awe na elimu kuanzia stashahada ya mojawapo ya fani zifuatazo: Kilimo/Mifugo/Mazingira/Maendeleo ya Jamii kutoka chuo kinachotambulika na serikali ya Tanzania.
3.      Awe na uwezo wa kutumia kompyuta.
4.      Awe muaminifu na muadilifu.
5.      Awe anajua kuendesha pikipiki na mwenye leseni ya udereva (Daraja A).
6.       Awe tayari kufanya kazi katika maeneo ya vijijini. Shirika la BUFADESO linafanya kazi na jamii ya wakulima na wafugaji wanaopatikana maeneo ya vijijini. Asilimia sabini na tano (75%) ya majukumu ya Afisa Mradi yatafanyikia maeneo ya vijijini walipo wanachama.

MUDA WA MKATABA:
Afisa Mradi wa Shirika atafanya kazi kwa Mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Mkataba wa ajira unaweza kuongezwa kutokana na utendaji kazi wa mtumishi.

Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma pamoja na taarifa binafsi (C.V) na ziwasilishwe kwa barua pepe au kupitia posta. 
Wanawake wenye sifa zinazohitajika wanahamasishwa kuomba nafasi hii na watapewa kipaumbele.

Maombi yatumwe kwa;
Mwenyekiti,
Bunda Farmers Development Support Organization,
BUFADESO,
S.L.P. 95,
Bunda,
Mara - TANZANIA.

Au kupitia Barua pepe: bufadeso@gmail.com

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/01/2018 saa kumi kamili jioni.

Limetolewa na;

BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA BUFADESO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO