"Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi," alisema Waziri Mkuu. Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.
Mkoa wa Mara umejikita katika kulima zao la Pamba ambalo ndio limekuwa zao la biashara kwa muda mrefu pamoja na changamoto zilizokuwa zinakabili kilimo cha zao hilo hapo nyuma zikiwemo changamoto za pembejeo na bei yenye tija. Katika msimu huu wa kilimo, kutokana na mikakati ya serikali, wananchi wengi wamehamasika kulima zao hili. Shirika la BUFADESO nalo limeandaa shamba la mfano lenye ukubwa wa ekari mbili lililoko kijiji cha Kunzugu, Kata ya Kunzugu wilayani Bunda. Pia wanachama wa shirika wamelima mashamba ya pamba binafsi kuanzia ekari moja na kuendelea.
Shamba la Mfano lililolimwa na shirika la BUFADESO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni