Leo
ni siku ya MAZINGIRA DUNIANI. Siku ya Mazingira Duniani huazimishwa duniani
kote kila mwaka, tarehe 5 mwezi wa Sita. Lengo la siku hii ni
Kauli
mbiu ya Kimataifa ya mwaka huu 2018 kidunia inasema “KOMESHA UCHAFUZI WA
MAZINGIRA UTOKANAO NA PLASTIKI” Leo la kauli mbiu hii ni kuhamasisha watu wote
kuachana na matumizi holela la plastiki yanayosababisha uchafuzi wa mazingira
ikiwemo ardhi, hewa na vyanzo vya maji kama maziwa na bahari. Uzalishaji na
matumizi ya kupindukia ya vifaa vya plastiki huathiri mazingira na bayoanuai na
viumbe akiwemo mwanadamu. Hivyo dunia anahamasishwa kuwa na harakati endelevu
za kulinda maisha ya viumbe na maliasili ili kuifanya dunia kuwa safi na yenye
mazingira bora kwa kutokuwa na uchafuzi wa hewa, ardhi, na ,maji utokanao na
matumizi holela ya vifaa vya plastiki. Kidunia maadhimisho ya siku hii ya
Mazingira Duniani yatafanyika nchini India. India imechaguliwa na Umoja wa
Kimataifa kutokana na harakati za muda mrefu za nchi hiyo katika kupambana na
matumizi holela ya plastiki. Kwa hivi sasa nchi ya India imeonyesha uongozi
bora katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi na ni nchi yenye mikakati thabiti
ya kuhamia kwenye uchumi utoao kiwango kidogo cha hewa ukaa.
Siku
ya Mazingira Duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1972 na sasa imekuwa ni
maadhimisho ya kimataifa yenye lengo la kuelimisha umma kuhusu masuala
mbalimbali yahusuyo mazingira.
Nchini
Tanzania Kauli mbiu ya mwaka huu ni “MKAA NI GHARAMA, TUMIA NISHATI MBADALA.
Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka kauli mbiu hii kutokana na kiasi
kikubwa cha maeneo ya Misitu yanayoharibiwa kwa ajili ya kupata mkaa. Takwimu
zinaonyesha hadi kufikia mwaka jana (2017) kiasi cha hekta 46,942 huharibiwa
kila mwaka. Uharibifu wa misitu unasababisha uwepo wa changamoto za kimazingira
kama vile ukosefu wa mvua unaoleta ukame;
hali ya jangwa na joto; upotevu wa viumbe hai mbalimbali na mimea ya
asili; uharibifu wa vyanzo vya maji na uchafuzi wa ardhi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni