Jumatano, 21 Desemba 2016

TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA AFISA MRADI

TANGAZO LA AJIRA YA AFISA MRADI
Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO) ni shirika lisilokuwa la kiserikali linalofanya kazi wilayani Bunda, Mara-TANZANIA. Shirika la BUFADESO lilianzishwa tarehe 27/02/2012 na limesajiliwa tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696 chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya kiserikali. Mpaka sasa shirika la BUFADESO lina wanachama vikundi 112 kutoka kata za Neruma, Guta, Hunyari, Mcharo, Nyamang`uta, Kabasa, Nyamuswa, Sazira, Wariku, Ketare na Kunzugu. 

DIRA YETU:                                                                                                                           
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda.
DHAMIRA   YETU:                                                                                                                              
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu.
Shirika la BUFADESO linakaribisha maombi ya ajira kwa nafasi ya AFISA MRADI kwa watanzania wenye sifa, na uwezo.

KITUO CHA KAZI: Wilaya ya Bunda

MUDA WA KAZI: Mkataba wa mwaka mmoja. Muda wa mkataba wa ajira unaweza kuongezwa kutokana na utendaji wa mtumishi.

MAJUKUMU YA AFISA MRADI:
Afisa Mradi wa shirika la BUFADESO atatekeleza majukumu yafuatayo:
1.    Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendeshwa ya shirika kwa kuzingatia bajeti na mipango kazi.
2.    Kutoa elimu na mafunzo ya mambo yanayohusu kilimo mseto, Kilimo biashara, Mabadiriko ya Tabia Nchi, Nishati Mbadala, Mazingira, Ujasiriamali, Usawa wa Kijinsia na mada nyingine zinazowalenga wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali.
3.    Kutoa mafunzo ya vitendo ya kilimo na ufugaji.
4.    Kufuatilia maendeleo ya vikundi wanachama wa shirika.
5.    Kusimamia vikao na mikutano ya vikundi wanachama na kutoa miongozo na maelekezo.
6.    Kuhamasisha vikundi vya wakulima na wafugaji masuala mtambuka.
7.    Kujengea uwezo jamii katika utekelezaji wa shughuli walizopanga.
8.    Kutengeneza mahusiano mazuri kati ya shirika, jamii, vikundi, asasi mbalimbali na serikali ili kufanikisha shughuli za maendeleo.
9.    Kuwajengea uwezo viongozi wa vikundi na wawezeshaji jamii katika kutekeleza shughuli zenye kuleta maendeleo endelevu.
10. Kuhamasisha na kufundisha shughuli za kuongeza kipato halali kwa jamii.
11. Kuwezesha uanzishwaji na uendelevu wa vikundi
12. Kuwakilisha shirika kwa Washika dau mbalimbali.
13. Kupanga, kutekeleza na kufuatilia shughuli za kila siku za vikundi wanachama.
14. Kutunza kumbukumbu za shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikundi wanachama na shirika.
15. Kutekeleza majukumu mengine anayopewa na Msimamizi wake au uongozi wa Shirika,

SIFA ZA MWOMBAJI:
1.    Awe Mtanzania.
2.    Awe na astashahada/stashahada ya masomo ya Kilimo/Mifugo/Mazingira/ Maendeleo ya Jamii kutoka chuo kinachotambulika na serikali ya Tanzania.
3.    Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
4.    Awe muaminifu na muadilifu.
5.    Awe anajua kuendesha pikipiki na mwenye leseni ya udereva (Daraja A)
6.    Awe tayari kufanya kazi katika maeneo ya vijijini. Shirika la BUFADESO linafanya kazi na jamii ya wakulima na wafugaji wanaopatikana maeneo ya vijijini. Asilimia sabini na tano (75%) ya majukumu ya Afisa Mradi yatafanyikia maeneo ya vijijini walipo wanachama.

MUDA WA MKATABA:
Afisa Mradi wa Shirika atafanya kazi kwa Mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Mkataba wa ajira unaweza kuongezwa kutokana na utendaji kazi wa mtumishi.

Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma pamoja na taarifa binafsi (C.V) na ziwasilishwe kwa barua pepe au kupitia posta. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 2 Januari 2017

Maombi yatumwe kwa;
Mwenyekiti,
Bunda Farmers Development Support Organization,
BUFADESO,
S.L.P. 95,
Bunda,
Mara - TANZANIA.
Barua pepe: bufadeso@gmail.com

Limetolewa na;
BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA
BUFADESO
  

TANGAZO LA AJIRA YA MUDA NAFASI YA MHASIBU

TANGAZO LA AJIRA YA MUDA NAFASI YA MHASIBU
(TEMPORARY ACCOUNTANT EMPLOYMENT)

Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO) ni shirika lisilokuwa la kiserikali linalofanya kazi wilayani Bunda, Mara-TANZANIA. Shirika la BUFADESO lilianzishwa tarehe 27/02/2012 na limesajiliwa tarehe 04/12/2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto makao makuu Dar-es-salaam kwa usajili namba 10NGO/00006696 chini ya sheria No 24 ya mwaka 2002 sehemu ya 12(2) ya mashirika yasiyo ya kiserikali. Mpaka sasa shirika la BUFADESO lina wanachama vikundi 112 kutoka kata za Neruma, Guta, Hunyari, Mcharo, Nyamang`uta, Kabasa, Nyamuswa, Sazira, Wariku, Ketare na Kunzugu. 

DIRA YETU:                                                                                                                          
Kuwa asasi imara yenye kuleta maendeleo endelevu ya kilimo kwa wakulima wilayani Bunda.

DHAMIRA   YETU:                                                                                                                              
Kujengea uwezo wakulima juu ya kilimo bora, chenye tija na endelevu.
Shirika la BUFADESO linakaribisha maombi ya ajira ya muda kwa nafasi ya MHASIBU kwa watanzania wenye sifa, na uwezo.

KITUO CHA KAZI: Wilaya ya Bunda

MAJUKUMU YA MHASIBU:
Mhasibu wa shirika la BUFADESO atatekeleza majukumu yafuatayo:
1.    Ataandika na kutunza vitabu vya mahesabu na kumbukumbu nyingine.
2.    Atapokea fedha yote inayoingia katika shirika na kufanya malinganisho ya fedha inayopokelewa na inayolipwa kila siku.
3.    Kufanya malinganisho ya hesabu za benki kila mwezi na kufanya ulinganisho wa fedha mkononi/kwenye kasiki kila siku.
4.    Kufanya masawazisho ya hesabu za mwisho wa mwaka na kuandaa hesabu ya mapato na matumizi ya mwaka.
5.    Kutayarisha taarifa kila mwezi, hesabu ya mapato na matumizi na kuiwasilisha kwa Mratibu pia atatoa ripoti ya kila robo mwaka (miezi mitatu) kwenye vikao vya Bodi.
6.    Kusaidia ukaguzi wa hesabu unaofanywa na wakaguzi.
7.    Ataandaa ripoti ya matumizi ya fedha kwa wafadhiri kila mwezi.
8.    Atasaidiana na viongozi wa shirika kufanya shughuli yoyote inayohusiana na fedha na mahesabu ya shirika.

SIFA ZA MWOMBAJI:
1.    Awe Mtanzania.
2.    Awe na astashahada/stashahada ya masomo ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambulika na serikali ya Tanzania.
3.    Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
4.    Awe muaminifu na muadilifu.
Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya taaluma pamoja na taarifa binafsi (C.V) na ziwasilishwe kwa barua pepe au kupitia posta. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 2 Januari 2017
Maombi yatumwe kwa;
Mwenyekiti,
Bunda Farmers Development Support Organization,
BUFADESO,
S.L.P. 95,
Bunda,
Mara - TANZANIA.
Barua pepe: bufadeso@gmail.com

Limetolewa na;
BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA
BUFADESO
  

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

Kilimo cha Mbaazi

Mazingira ya kustawi
Ni mmea wenye mizizi mirefu kwenda chini, na huweza kuongeza nitrojeni
Huhitaji mazingira ya joto, kuanzia joto 25-40 sentigrade, haipendi baridi hivyo piga vizuri hesabu zako ni ,muda gani unataka kupanda hadi kuvuna. Kwa tanzania hapa maeneo mengi ya sehemu zenye joto yanakubali mazao haya
Ni mimea inayoweza kuchanganywa na ulezi, au mtama na mahindi

Nafasi ya upandaji
MITA 1 KWA 1.5M , KUTOKA MCHE HADI MCHE 1M, NA MSTARI HADI MSTARI 1.5 M, Katikati yake unaweza unaweza kuchanganya na mazao mengine, kama vile maharage, au hata Mahindi

MUDA WA KUOTA MBEGU
Tangu kupanda mbegu hadi kuota huchua siku 4 hadi 21, na baada ya hapo mimea huanza kukua polepole, hivyo hakikisha unazuia magugu

MUDA WA KUKOMAA
Tangu kupanda hadi kutoa maua,huchukua siku 60 hadi 80, na baada ya maua huchukua siku 50-75 kutengeneza mbegu zilizokomaa, hivyo huchukua kati ya miezi 5 hadi 6 kukomaaa

IDADI YA MEBEGU KWA EKA 1
KILO 10 hutosha kwa ekari moja, kama unaweka mbegu mbilimbli kwa shimo, na kilo 5 hutosha kwa ekari moja kama unaweka moja moja kwa shimo

WADUDU WA HARIBIFU
1. Funza wa matunda
2. Funza wa kukata mimea ikiwa michanga
3.Mnyauko (Fusarium Wilt)
5. Ukungu-Fangasi
Madawa ya kuzuia waduu
. 1. Karate 2. Match, 3. Phyrinex, 4. uduall, 5. Seecron, Moja wapo ya hizo dawa zitakusaidia sana, LITA 3 ZA DAWA ZITAKUTOSHA,  

Madawa ya kutumia kuzuia ukungu ni kama vile
1. Ridomil Gold 2. Ebony (Mancozeb +Metalaxyn), 3, Ivory, 4. Nordox etc Moja wapo ya hizo dawa zitakusaidia sana, LITA MBILI /KILO MBILI ZA DAWA ZITAKUTOSHA

MBOLEA ZA KUPANDIA
Wakati wa kupanda, mboleya kama vile Yara Miller Winner, au NPK, DAP, MiNJINGU AU TSP, zitakufaa, angalu mifuko 2 kwa eka 1

WAKATI WA KUKUZIA
Utahitaji mbolea kama vile, CAN, UREA, AU NPK, Au Yara Miller winner, Mifuko 3 itakutosha

MAVUNO
Mavuno kwa eka moja ni kati ya tani 1 hadi 4, yaani ( gunia 10 hadi 40 za uzito wa kilo 100). Hii inategemeana na rutuba ya ardhi katika shamba husika.












 na
Baraka KAMESE
Mratibu-BUFADESO

Kauli mbiu yetu

BUFADESO kwa maendeleo ya wakulima

MUHIMU

Makala na picha zinazochapishwa katika blogu hii ni kwa ajili ya taarifa na kumbukumbu za Shirika la Bunda Farmers Development Support Organization (BUFADESO)
Hairuhusiwi kutumia yaliyomo katika blogu hii (HASA PICHA) kwa shughuli zozote bila ruhusa ya mmiliki wa blogu hii ambaye ni BUFADESO